Na Innocent Mwalo.
Ukiwa ni mkakati wa kukabiliana na tatizo la utapiamulo wilayani hapa, Kamati ya Lishe ya Wilaya, mnamo tarehe 27/01/2021 imefanya kikao chake cha robo pili kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 na kuweka mikakati kadhaa wa kadhaa yenye lengo la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athali za utapiamlo wilayani hapa.
Katika taarifa aliyoiwasilisha kwa wajumbe wa kikao hicho, Mratibu wa Lishe Wilayani hapa Bi. Lustika Mgumba alibainisha baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha robo ya kwanza kiliachoanza mwezi Oktoba 2020 mpaka Januari 2021 ya kwamba jumla ya akinamama wajazito 9897 sawa na asilimia 64 waliweza kupata madini chuma ikiwa ni afua ya kupambana na tatizo la athali za utapiamulo kwa watoto wanaotarajiwa kuzaliwa.
Kali kadhalika Bi. Lustica alibainisha mafanikio kadhaa wa kadhaa yaliyofikiwa katika kipindi cha robo hiyo ikiwa ni pamoja na jumla ya watoto 70,0348 kati ya 731359 sawa na asilimia 92.2 kuweza kupata dawa za vitamin A, pamoja na jumla ya kaya 18113 sawa na asilimia 56 ya kaya 32306 za walengwa zilitembelewa kupewa elimu ya lishe na wahudumu ngazi ya jamii.
Aidha taarifa nyingine zilizowaslishwa katika kikao hicho kupitia Idara na wadau wengine katika sekta ya lishe wilayani hapa zilieleza baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa katika kuondoa tatizo la utapiamulo wilayani hapa, ambapo taarifa ya Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Wilaya iliyowasilishwa na Bw. Deogratius Kanyonyi, pamoja na mambo mengine iliyobainisha kuwa vikundi vyote vilivyokopeshwa mikopo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu vimeweza kuanzisha miradi mbalimbali kama ufugaji na ile ya kilimo cha bustani ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo.
Mbali na mafanikio anuai yaliyotajwa na wajumbe waliowasilisha taarifa kuzihusu sekta za Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Afya, Maendeleo ya Jamii, Maji, Mipango naTASAF pamoja na yale ya wadau wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na viongozi wa dini kuhusu sekta hiyo ya lishe, wajumbe walionesha kushtushwa na takwimu zilizotolewa na Idara ya Elimu Msingi ambazo zilibainisha ya kwamba kati ya shule za msingi 119 zilizopo wilayani Karagwe, shule 9 wanafunzi wake walikuwa hawapati huduma ya uji/chakula shuleni kwa robo ya Oktoba- Disemba 20202.
Kadhalika takwimu zilionesha kuwa kati ya shule hizo 09; shule 03 ni kutoka kwenye kata ya Kiruruma, 01 Kata ya Nyakakika, 02 Kata ya Kituntu, 01 Bweranyange, 1 Kanoni huku nyingine 1 ikitoka katika Kata ya Kibondo.
Aidha wajumbe walioneshwa kushangazwa sana na takwimu za Idara ya Elimu Msingi zilibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 36,722 sawa na asilimia 49.67 ya wanafunzi wote 73,923 waliosajiliwa katika shule za msingi wilayani kuwa ndio pekee wanaopata uji/chakula shuleni.
‘’Kuanzia sasa ni lazima tubuni kampeni mbalimbali za kuhamasisha Elimu ya kujitegemea kwa shule zilizobainika kuwa na maeneo makubwa ya kilimo ili shule hizo ziweze kuzalisha chakula chake zenyewe’’, alisisikika mmoja wa wajumbe akipendekeza hilo liwe moja ya maazimio ya kikao hicho.
Kwa upande mwingine baadhi ya afua zilizopendekezwa na wajumbe hao ili kukabiliana na changamoto hiyo ilikuwa ni kuendelea kuhamasisha suala la lishe mashuleni kupitia vyombo vya habari, michezo mashuleni, vikundi vya kijamii na nyumba za ibada.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.