Kamati ya fedha, uongozi na mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Karagwe imefanya ziara ya kujifunza namna ya kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani. Ziara hiyo imefanyika kati Halmashauri za wilaya za Kilosa, Mvomero na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Mhe. Wallace Mashanda, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe amesema kuwa, lengo la ziara ni kujifunza namna ya kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani. Kujifunza huwa hakuna mwisho na Halmashauri siyo kisiwa. Kuna vyanzo vingine vya mapato ambavyo havitozi katika Halmashauri ya wilaya ya Karagwe wakati wengine wanavitoza.
Katika ziara hiyo ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa kuona vyanzo vya mapato vinavyokusanywa, kupitia sheria ndogo za Halmashauri hizo na kuona namna timu za mapato zinavyofanya kazi.
Aidha, ziara hiyo ilijumuisha waheshimiwa madiwani 9 ambao ni wajumbe wa kamati ya fedha, uongozi na mipango pamoja na watalaam 9.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.