Na Innocent E. Mwalo.
Pamoja na nia ya kuhakikisha afya za wananchi zinaboreshwa kwa kuwa na bima za kuwawezesha kupata matibabu, Kamati ya Elimu, Afya na Maji katika kikao cha robo ya tatu ya 2020/2021 cha tarehe 19/04/202, imetoa angalizo kwa Idara ya Afya wilayani hapa kuboresha utoaji wa huduma ili kuweza kuwavutia wananchi wengi zaidi kujiunga na mfuko huo.
Ushauri huu ulitolewa na wajumbe wa kikao hicho kufuatia takwimu zilizowasilishwa na Mkuu wa Idara ya Afya, Dkt. Ramadhani Hussein, kwenye kikao hicho ambazo zilionesha kuwa kwa kipindi cha Januari mpaka Machi, 2021, kaya 634 sawa na asilimia 0.7 tu ndizo zilizosajiwa kwa kipindi hicho.
Baada ya kupokea takwimu hizo, wajumbe wa kamati hii kwa nyakati tofauti, walitoa ushauri na maelekezo kwa menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya kuongeza jitihada za kuhamasisha wananchi juu ya kuona umuhimu wa kujiunga na mifuko hii ya afya ili kujihakikishia huduma za afya pindi wanapopata shida ya maradhi.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati hii, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyakahanga, Mh. Charles Beichumila aliungana na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya katika kupaza sauti kwa serikali kuu juu ya kuchelewa kuletwa na kupokea fedha ambazo ni gawio kwa ajili ya kununua dawa kwa ajili ya wanufaika wa mfuko.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.