Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imesaini mkataba wa miaka minne na Jimbo la Furth wenye thamani ya shilingi za kitanzania million 634 kwa lengo la kudhibiti taka ngumu ilikuimairisha utunzaji wa mazingira mamlaka ya mji mdogo wa Kayanga
Zoezi hilo la utiaji saini limefanyika tarehe 23 julai 2024 katika ukumbi wa ELCT Wilayani Karagwe na kushudiwa na waheshimiwa madiwani, wakuu wa Idara na Vitengo, baadhi ya watumishi wa umma, waandishi wa habari pamoja na wawakilishi kutoka jimbo la furth nchini Ujerumani
Mkataba huo umetiwa saini na Mkurugenzi mtendaji Bi.Happiness Msanga, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe; Wallace Mashanda, Mwanasheria wa Wilaya Ndg; Saul Nyamunda pamoja na meya wa jiji la Furth nchini Ujerumani Ndg; Andrea Horsche
Akizungumza mara baada ya utiaji saini, mwenyekiti wa Halmashauri Mhe; Wallece Mashanda amelishukuru jimbo la Furth kwa mchango wao na kuwa mdau wa maendeleo Karagwe nakuahidi kuwa pesa hizo zitatumika kama walivyokubaliana katika mkataba. Pia aliongeza kuwa, Halmashauri itachangia asilimia 10 ya mkataba huo fedha kutoka mapato ya ndani ili kuhakikisha utekelezaji wa utunzaji mazingira unaimarika
Kwa upande wake Bwana Andrea amesema kuwa jimbo la furth lipo tayari kutekeleza mradi huu kwa ushirikiano kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho
“Kwa Ushirikiano tunaweza kufanikisha mambo makubwa kwa ajili ya Manispaa zetu, mazingira yetu kwa ajili yetu na kizazi kijacho na tunasubiri kwa hamu hatua zijazo za utekelezaji na ushirikiano zaidi” alisema Adrea
Aidha Diwani wa kata ya Ihanda Mhe: Ladislaus Kamuhangile amelishukuru jimbo la Furth kwa mradi huo, na kuomba waendelee kushirikiana kwa mambo mengine ya kuleta maendeleo Karagwe
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.