Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera Ndg: Dr. Amon David Mkoga Leo Mei 4, 2024 amekutana na kuzungumzana na Timu ya Wataalamu ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe (CMT), Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji, Makatibu Tarafa na maafisa Ugani kwa lengo lakufahamiana na kuwekeana mikakati ya utendaji kazi na ukusanyaji wa Mapato.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Angaza amewataka watendaji wa kata, Watendaji wa vijiji, na Maafisa ugani kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato, kusimamia miradi, kusikiliza na kutatua kero zawananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka kuzalisha kero mpya na kudhibiti magendo ya Kahawa.
"Katika kipindi chote nitakachokuwepo Karagwe vipaumbele vyangu ni vinne ukusanyaji wa mapato, Usimamizi mzuri wa Miradi ya serikali, kutatua kero za wananchi na ushirikiano wa pamoja ambavyo nitavitumia kupima utendaji kazi wenu ambavyo mkifanya vizuri nyie ni sifa kwa Halmashauri na wala hamtagombana na mimi zaidi ya kuwa marafiki na naomba ushirikiano wenu twendeni tukafanye kazi kwa kasi mpya,"amesema Mkurugenzi Dr. Mkoga.
Pia katika kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mh: Julius Kalanga Laiser na kuwaomba Watumishi kuwahi kazinina kutimiza majukumu yako kama mtumishi wa umma na Mtendaji wa kata ndiyo bosi wa kata kwa hiyo watumishi wote ndani ya kata walete taarifa ya Kahawa kwa Mtendaji wake wa kata.
“Tumpe ushirikiano Mkurugenzi wetu Dr. Mkoga ni mtu aliyenyooka na mpenda haki tumuamini atatenda miujiza na Halmashauri yetu itasonga mbele” Alisema Mkuu Wilaya Mhe: Laiser.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.