DC LAIZER AWATAKA WANAWAKE WA KARAGWE KUJIIMARISHA KIUCHUMI.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe: Julius Kalanga Laizer amewataka Wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kutumia fursa zilizopo Wilayani humo ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ili waweze kujiimarisha kiuchumi.
Akizungumza mapema leo Tarehe 08/03/2025 wakati akitoa hotuba fupi ya maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani katika Wilaya ya Karagwe, ambayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Kagutu, Kata ya Ndama Wilayani humo.
"Moja ya changamoto hapa Karagwe ni ukatili wa kijinsia na kimama wengi wamekua wahanga kwasababu ya umaskini, kama mwanaume anajua huna unachoongeza kwenye familia lazima akutese. Uchumi ni nguzo imara kwenye familia zetu niombe Wanawake mfanye kazi na biashara ili muwe vizuri kiuchumi" Alisisitiza mhe. Laizer.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya siku ya Wanawake 2025 Bi. Ainess Samuel amewapongeza Wanawake wote Nchini kwa maadhimisho hayo na juhudi wanazofanya kwenye kuhakikisha wanashiriki kwenye shughuli za kimaendeleo Na kuwasisitiza kujitafutia vipato vyao ili kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia ambao kwa kiasi kikubwa unasababishwa na wao kuwa wategemezi.
Aidha, Maadhimisho hayo yaliambatana na uzinduzi wa awamu ya kwanza wa utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ambapo hundi ya kiasi cha shillingi Millioni 127 kwa vikindi 11 (Wanawake vikundi 9, vijana 1 na Watu wenye ulemavu 1). Vilevile, Maadhimisho hayo yalipambwa na mashairi , muziki pamoja na mabanda mbalimbali ikiwemo banda la ya upimaji afya na lishe, banda la dawati la jinsia na msaada wa kisheria pamoja na banda la wajasiriamali .
Hata hivyo, Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe haki, Usawa na Uwezeshaji yalienda sambamba na Kufanya matendo ya huruma kwa wanafunzi wakike walio kwenye mazingira magumu kwa kutoa misaada ya hali na mali, kuboresha nyumba ya mama mzee kijiji cha kagutu, kushiriki shughuli za kujitolea kwenye miradi ya maendeleo ya jamiii, kutoa elimu kwa kushirikiana na SIDO ili kuongeza mnyororo wa thamani kwenye uzalishaji kwa Wanawake wajasiriamali.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.