DC LAIZER AONGOZA USAFI NA BONANZA MAIDHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe; Julius Kalanga Laizer ameongoza zoezi la kufanya usafi mazingira na bonanza katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania leo tarehe 09 Desemba 2024.
Maadhimisho hayo ya miaka 63 Wilaya ya Karagwe yalianza kwa kufanya usafi wa mazingira sehemu mbalimbali za mji wa Kayanga uliongozwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi; Happiness J. Msanga kwa kushirikiana na Watumishi wote na Wananchi wa Wilaya ya Karagwe kwa maeneo ya Stendi ya mabasi Kayanga, Soko la Kayanga na Ofisi ya Kata ya Kayanga.
Baada ya zoezi la usafi Mhe.Laizer aliongoza Watumishi na Wananchi kuelekea uwanja wa Bashungwa kwa ajili ya Bonanza la michezo ambalo lilihusisha michezo mbalimbali kama vile mpira wa pete na Mpira wa Miguu ambapo timu ya ulinzi na usalama ilishindana na watumishi Halmashauri. Pia kulikua na zoezi la kuendesha baiskeli kuzunguka uwanja huo zote hizi zikiwa ni shamrashamra za kusherekea miaka 63 ya uhuru tangu Tanzania ilipotangazwa rasmi kuwa huru mwaka 1961 na aliyekua Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere.
Aidha, Mhe.Laizer amesema kuwa Wananchi wa Wilaya ya Karagwe wanaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote nchini kuenzi na kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru kwa Amani, Mshikamano na Ushirikiano uliyobeba kauli mbiu isemayo “Uongozi madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi.Hapiness Msanga amewapongeza Watumishi na Wananchi wote waliojitokeza kushiriki maadhimisho hayo kikamilifu na kwa mshikamano kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Hata hivyo, Maaadhimisho haya hufanyika kila mwaka tarehe 09 Desemba kulingana na maelekezo yanayotolewa na Rais ambapo kwa mwaka huu Mhe. waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa Rais ameelekeza Maadhimisho haya yafanyike katika ngazi ya mikoa na Wilaya kwa kufanya shughuli za kijamii ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile kwenye Masoko, Hospitali, pamoja na mashindano ya michezo mbalimbali, makongamano na midahalo ya kujadili maendeleo endelevu ambayo nchi yetu imefikia katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.