Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe: Julius Kalanga Laiser Amesikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Tarafa ya Nyakakika na kuzitatua papo hapo ambapo Mkutano huo umefanyika katika Kata ya Kibondo kijiji cha Nyakaiga leo April 2, 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe: Julius K. Laiser
Mhe: Laiser aliongozana na wataalam wa taasisi za kiserikali na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ambapo Mkuu wa Wilaya ameanzisha kliniki tembezi ya kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wengi katika Tarafa Tano na Kata 23 za Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.
Katika Mkutano huo Wananchi wa Tarafa ya Nyakakika Wilayani Karagwe Mkoani Kagera wameomba kutatuliwa changamoto ya huduma ya Maji na Umeme ambayo imedumu kwa muda mrefu katika baadhi ya vijiji ambavyo havijapata huduma ya maji na umeme na kusababisha shughuli za uzalishaji mali kukwama katika kitongoji Cha Kabindi B, Kijiji Cha Kahio na kijiji cha Nyakaiga.
Wakizungumza katika mkutano wa adhara ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe kwa lengo ya kuisikiliza kero za wananchi na kutoa majibu April 2 mwaka huu wamesema kwa Sasa vipo baadhi ya vijiji bado havijawashiwa na kumuomba mkuu wa Wilaya kuwasaidia kwa kuwatumia wataalam kuwapatia huduma hiyo
Akiuliza swali katika mkutano huo Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji John Katunzi Kahio na Venant Evarister mkazi wa kitongoji Kabindi B wamehoji ni lini umeme utawashwa kwa wananchi wengine kutokana tayari nguzo zimesimikwa kwa muda mrefu na nyumba tatu ndo zimewashiwa umeme
Akitoa majibu Meneja TANESCO Wilaya ya Karagwe Kitila Anania amesema awali Mkandarasi alipewa kilometa 1, na mpaka kufikia Sasa ameongezewa kilometa mbili ili kuwaunganishia wananchi na kufikia jumla ya wateja 66 kupata umeme
Pia alitolea Majibu amesema katika kitongoji Cha Kabindi hakikupata nishati ya Umeme katika awamu ya kwanza REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza na kukamilika mwaka Jana hivyo katika maeneo ambayo hayakufikiwa na umeme wapo tayari kwenye mpango na watafikiwa na umeme.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.