Zaidi ya Mabinti 33,720 wenye miaka 9-14 wilayani Karagwe wanatarajia kupata chanjo ya HPV dhidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kupitia kampeni ya siku tano kuanzia april 22 mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa na Mganga mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dr. Agnes Mwaifuge katika kikao cha kamati ya Afya Msingi PHC kilichoketi katika ukumbi mdogo wa ofisi za mganga mkuu Hospitali ya Wilaya Karagwe Nyakanongo.
Dr: Mwaifuge amesema kuwa kampeni hhi ya utoaji chanjo itafanyika katika shule za msingi na Sekondari na vituo vya tiba kwa walengwa kwa siku tano kuanzia april 22 hadi 26 mwaka huu ingawa zoezi hilo litaendelea mpaka mwezi wa 12, na kuwa watoto zaidi ya 33720 watafikiwa na kuchanjwa.
Ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa dozi ya chanjo hiyo ni moja bali kwa mabinti wanaoishi na virusi vya Vvu ambao wao watapewa dozi tatu kutokana na kinga yao kuwa chini.
Aidha Mwenyekiti wa kikao hicho ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Laizer ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea Chanjo hii ya saratani ya mlango wa kizazi ili kuwakinga watoto wetu wa kike dhidi ya ugonjwa huu hatari.
Pia Mhe: Laiser amekemea baadhi ya imani potofu zinazoendekezwa na baadhi ya wananchi huku akiitaka idara ya Afya kuendelea kutoa elimu sahii juu ya umuhimu wa chanjo kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari kwani chanjo ni salama na haina madhara yoyote na wazazi wawahimize watoto wao kupata chanjo hii ambapo Mkoa unatarajia kuchanja watoto wapatao 271,650.
Nao Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wameahidi kutoa ushirikiano ili zoezi hilo liweze kufanikiwa.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.