BUGENE SEKONDARI YAKIMBIZANA KEMEBOS, NYAISHOZI KITAALUMA 2022
Shule ya sekondari ya Bugene ya Halmashauri ya wilaya ya Karagwe imeshika nafasi ya tatu (3)kimkoa katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita 2022. Shule hiyo inataasusi za HGE,HGL,HGK,HKL na CBG.
Jumla ya wanafunzi 192 waliofanya mtihani wa kuhitimu kidato cha sita 2022 na kati ya hao, wanafunzi 139 wamepata daraja la I (division one) na wanafunzi 53 walipata daraja la II (division II).
Bw. Leonard Rwazo, Mkuu wa shule ya sekondari Bugene amesema kuwa, “ … tumejipanga na tunaendelea kuweka mikakati ya kufuta daraja la pili katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita 2023. Kwa sasa shule tunazokimbizana nazo kitaaluma ni Kemebos na Nyaishozi ”. Alisema Bw. Rwazo
Aidha, wanafunzi nao wanaendelea kujiandaa vizuri kwalengo la kuendeleza ufaulu mzuri. Kwa kipindi cha miaka saba mfululizo, shule ya sekondari Bugene imekuwa ikipanda kielimu. Kila mwaka inazidi kufanya vizuri zaidi. Kwa mfano, mwaka 2021 kulikuwa na wanafunzi 206 na kati hao, waliopata daraja la kwanza ni 85, daraja la pili 92 na daraja la tatu 29. Kwa mwaka 2020, waliopata daraja la kwanza 31, daraja la pili 79, daraja la tatu 42 na daraja la nne 01.
Pia kwa mwaka 2019, Shule ya sekondari Bugene ilikuwa na watahiniwa 127 wa kidato cha sita. Wanafunzi 39 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 58 daraja la pili, 29 daraja la tatu na 01 daraja la nne. Kwa mwaka 2018, daraja la kwanza 10, daraja la pili 61, daraja la tatu 43, daraja la nne 04 na daraja la sifuri 01.Kwa mwaka 2017, daraja la kwanza 13, daraja la pili 41, daraja la tatu 22 na daraja la nne 02 na kwa mwaka 2016, daraja la kwanza 04, daraja la pili 22, daraja la tatu 16, daraja nne 01 na daraja sifuri 02.
Kwa mkoa wa Kagera, shule ya kwanza ni Kemebos (shule binafsi na yakwanza Kitaifa), shule ya pili kimkoa ni Nyaishozi (shule binafsi na yasaba Kitaifa) na shule ya tatu ni Bugene sekondari (ya serikali na ya 57 Kitaifa).
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.