Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Karagwe Mhe: Wallace Mashanda ameipongeza kamati ya ukusanyaji mapato ya Halmshauri ya Wilaya ya Karagwe kwa usimamizi mzuri. Kauli hiyo aliitoa wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kinachohitimisha kipindi cha Robo ya Tatu katika Mwaka wa fedha 2023 / 2024. Kikao hicho kilifanyika Mei 07 na 08, 2024 Mwaka huu katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya (Angaza).
Mpaka kufikia Aprili 30, Mwaka huu (2024) Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imeshakusanya Mapato kwa Asilimis 75.5 Mapato hayo yamekusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vya Mapato vilivyopo Halmashauri huku ikibakiza Asilimia 24 ya ukusanyaji wa Mapato ili kufikia lengo iliyojiwekea katika Mwaka wa fedha 2023 / 2024.
“Mpaka mwezi March mwaka huu mapato yasiyolindwa yamekusanywa kwa asilimia 73.4 huku mapato lindwa yamekusanywa kwa asilimia 75.05” Alisema Mhe: Mashanda ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani. Mhe. Mashanda alisisitiza kuwa kuongezeka kwa mapato katika Halmashauri kutasaidia Halmashauri kuwa na fedha za kutosha zitakazosaidia katika utekelezaji wa Miradi ya Mendeleo.
Pia Mh: Mashanda Ameongeza kwa kuwataka watendaji kuhakikisha wanasimamia vizuri na kuwaeleza wananchi fedha zinazoletwa katika ngazi ya kata kutoka serikali kuu na Halmashauri ili wananchi kutambua shughuli zinazoendelea kutekelezwa katika maeneo yao
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera Mhe: Julius Kalanga Laiser wakati akitoa taarifa ya serikali amewataka viongozi kusimamia mapato ya halmashauri ikiwa ni pamoja na kusimamia zao la kahawa pamoja na kuzuia suala la uvunaji wa kahawa mbichi “kwa yeyote atakaye kamatwa anavuna Kahawa Mbichi na Kwa Magendo Kahawa yake tutaitaifisha na siyo kutozwa faini tena ili kukomesha masuala haya ya utoroshwaji wa Mapato ya Serikali”
Aidha Halmashauri ya wilaya ya Karagwe kwa kushirikiana na wadau was mazingira imetembulisha mradi wa Hifadhi Mazingira Karagwe (Greening Karagwe Project) utakaogharimu zaidi ya shilingi bill 6.067 ambao utatekelezwa kwa kipindi Cha mwaka 2024/2025 na kukamilika 2028 Hadi 2029.
Akitambulisha mradi huo kupitia kikao Cha Baraza la madiwani Cha robo ya tatu ya mwaka 2023/2024, Afisa Maliasili Na mazingira Ndg: Rajab Khasimu amesema kwa kushirikiana na wadau wa mazingira utasaidia kutatua kero za uharibufu wa mazingira
Khasim amesema wanatarajia mradi huo utatekelezwa kuanzia shule za msingi 125, sekondari 36, vituo vya afya 50, wananchi 71,000 pamoja na maeneo mengine ya wazi na mji wa Kayanga
Wakichangia Mara baada ya wasilisho la utekelezaji wa mradi huo, Diwani wa kata ya Rugu Adrian Kobushoke, Zidina Murishidi kata ya Kituntu na Diwani wa kata ya Nyakabanga Jastine Ntikaligaile wamewapongeza wadau kukubali kuungana kwa pamoja na kupendekeza kuruhusu wadau wengine wa mazingira kuendelea kujitokea ili kuungana kwa pamoja katika kukabiliana na uharibu wa mazingira ambayo umefanyika kwa kiwango kikubwa Kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji
Akitaja maazimio ya Pamoja Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mhe: Wallace mashanda amesema wanapaswa kuzingatia usimamizi mzuri wa sheria za misitu na vyanzo vya maji, kubainisha maeneo katika ngazi ya kata, vijiji ili kupanda miti, pamoja na kuhakikisha Kila shule ya Msingi na Sekondari kuwepo kwa vitalu vya miti na klabu za Mazingira.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.