Na Innocent E. Mwalo.
Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya Karagwe, mnamo Machi 10, 2021 kwa kauli moja limepitisha kiasi cha shilingi 45,229,359,445.00 ikiwa ni bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Kabla ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, waheshimiwa madiwani walipata wasaa wa takribani siku mbili wa kujadili vyanzo mbalimbali vya mapato na matumizi hayo ya Halmashauri ya wilaya ambapo taarifa mbalimbali zilizowasilishwa na kujadiliwa katika baraza hilo zilionesha na kuchanganua ya kuwa kati ya kiasi hicho cha shilingi 45,229,359,445.00 kitahusisha ruzuku za matumizi ya kawaida (OC) kiasi cha shilingi 1,025,855,000, mishahara kiasi cha 26, 962, 644,860, ruzuku za miradi ya maendeleo 9, 439, 598,325 na mapato ya ndani yatakuwa ni shilingi 2,671,904,000.
Kwa upande mwingine, taarifa na majadiliano zilionesha ya kuwa Halmashauri ya wilaya inatajia kupata na kutumia kiasi 230,000,000 ikiwa ni jitihada jamii huku kiasi kingine cha shilingi 4,563,433,923 kikiwa ni mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Pamoja na baadhi ya madiwani kuridhishwa na bajeti hiyo, (hii ni kupitia maoni mbalimbali waliyoyatoa kwenye mjadala huo), baadhi madiwani akiwemo Magnus Cheusi ambae ni diwani anayetoka katika kata ya Kibondo waliomba ufafanuzi wa kwanini baadhi ya zahanati zinawatoza akina mama wajaziwazito kiasi cha shilingi laki tatu wakati wa kujifungua ambapo majibu ya menejimenti ya Halmashauri ya wilaya kupitia kwa mganga mkuu wa wilaya Dkt. Ramadhani Hussein alibainisha kuwa sera ya afya haijabadilika na hivyo alitoa rai kwa wafawidhi wa zahanati na vituo vya afya kuacha mara moja tabia ya kuwatoza wanawake wajawazito wanapo hitaji huduma.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.