BARAZA LA MADIWANI NA WAKUU WA IDARA WA TARIME DC WAFANYA ZIARA YA MAFUZO YA ZAO LA KAHAWA KARAGWE DC
Baraza la Waheshimiwa Madiwani likiongozwa na Mbunge wa Tarime Mhe. Mwita Waitara, Mkurugenzi Mtendaji, na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wamefanya ziara ya mafunzo ya Siku moja ya zao la Kahawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwa lengo la kujifuza namna ya kuongeza thamani kwa zao la kahawa kuanzia linapoanza kupandwa mpaka linapofikishwa sokoni kwa ajili ya mnada.
Ziara hiyo iliyofanyika Tarehe 16/12/2024 iliongozwa Mkurugezi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Tarime Ndg. Solomon Shati ulipokelewa na Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kiruruma Mhe. Evalista Tinkamanyile Sylivesta pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi. Beatrice Laurent.
Aidha, ziara hiyo ilianza kwa mafunzo ya nadharia na uwasilishwaji wa taarifa kuhusu zao la kahawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe yaliyofanyika katika Ukumbi wa Angaza Wilayani humo ambapo maswali mbalimbali yaliulizwa na kupewa majibu pia kulifanyika majadiliano na kubadilishana ujuzi katika kuongeza uthamani wa zao la kahawa na uzalishaji wa tija.
Pia, Ziara hiyo ilihusisha mafunzo ya vitendo ambapo msafara huo ulipata nafasi ya kutembelea kitalu cha miche ya mibuni (kahawa), Shamba la kahawa lilipo eneo la Kihanga pamoja na kiwanda cha kusindika kahawa (KDCU). Vituo vyote walivyopita walipatiwa mafunzo ya vitendo yaliyoongozwa na Kaimu Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Ndg. Dominick Yustadi.
Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mhe. Simon Kiles Samuel ameushukuru Uongozi wa Wilaya ya Karagwe kwa mapokezi waliyopata na mafunzo waliyopewa ambayo ndio msingi wa ziara yao. Aliongeza kuwa, kupitia mafunzo hayo wataweza kuzalisha na kuongeza thamani ya zao la kahawa kwenye Halmashauri yao.
“Mafunzo tuliyopata hapa tutayatumia vizuri katika kuongeza thamani ya zao la kahawa kwenye Wilaya yetu, tulichagua kuja hapa kwa sababu tuliamini tunaweza kujifunza vingi kutoka kwenu. Tunatamani siku moja na nyie mfanye ziara kwetu tunahakika hamtatoka bure sisi ni marafiki tudumishe urafiki wetu” alisema Mhe.Simon.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.