Na Innocent E. Mwalo.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya, kupitia Mkutano wake wa kipindi cha robo ya nne, Aprili - Juni, 2021, uliofanyika katika Ukumbi wa Vijana Rafiki Angaza, Julai 27/28, 2021, kwa kauli moja umemfukuza kazi Bwana Nelson Justinian Thadeo, aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Omkakajinja katika kata ya Rugera, kwa makosa makubwa mawili ikiwemo la kuuza ardhi ya kijiji yenye ukubwa wa takribani ekari 30 pamoja na kughushi saini ya mtendaji wa kata hiyo ilikufanikishia lengo hilo.
Mwingine aliyechukuliwa hatua na Baraza hilo ni Mtendaji wa Kijiji cha Kibwera, Bwana Dawson Tinkasimile ambaye uamuzi uliofikiwa na Barazala madiwani kwamba alipewa karipio kali kufuatia kushindwa kutekeleza majukumu yake pamoja na kushindwa kuitisha mkutano wa kijiji kwa lengo la kusoma mapato na matumizi ambapo uamuzi huo wa Baraza la Madiwani ulitangazwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mh. Wallace Mashanda mbele ya wajumbe na wananachi wote waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.
Katika hatua nyingine, Mkutano wa Baraza la Madiwani umejadili ajenda mbalimbali zilizowasilishwa kwenye mkutano huo ikiwemo taarifa mbalimbali za kamati za kudumu za Halmashauri ya wilaya kama vile kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira pamoja na Kamati ya Kudhibiti UKIMWI ambapo mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hizo waheshimiwa madiwani walijadili na kuweka maazimio kadhaa kwa menejimenti ili kuongeza kasi ya utendaji katika maeneo hayo.
Katika kuchangia taarifa hizi ikiwemo taarifa ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, waheshimiwa madiwani kwa nyakati tofauti wamepongeza jithada zilizofikiwa na Halmashauri kwa menejimenti kuweza kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 108 za lengo lililowekwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
‘’Tunapongeza jitihada zilizofikiwa na Halmashauri katika suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambapo kwa kipindi hiki cha mwaka wa fedha mmekusanya kiasi hicho, wito wangu kwenu ni kuongeza juhudi na maarifa kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa mwaka huu wa fedha ambapo dalili zinaoonesha kuwa mapato ya kahawa yatakuwa kidogo ukilinganisha na makadirio tuliyoyafanya kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha 2021/2022’’, alisisitiza Mh. Mashanda.
Wajumbe wengine waliochangia kwa hisia kali taarifa za kamati hizo ikiwemo ile ya Kamati ya Elimu, Afya na Maji ambayo ilionesha changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa walimu takribani 986 kwa shule za msingi zilizopo wilayani hapa na changamoto nyingine ikiwa ni ile ya lishe duni kwa baadhi ya kaya hali inayopelekea wilaya hii na mkoa wa Kagera kwa ujumla kubainishwa kama mikoa yenye changamoto kubwa ya watoto wenye utapiamulo, Mh. Dawson Byamanyirohi, Diwani wa Kata ya Rugera na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya alisema ‘’Inawezekana changamoto yetu ya kukosa walimu wapatao 986 ikawa haijaripotiwa kwa namna mkoa na taifa kuliona hili kama tatizo kubwa kwa kulinganisha na mikoa mingine hivyo basi tunaagiza menejimenti kufanya ufuatilia kuptia kwa katibu Tawala wa mkoa juu ya takwimu za wilaya nyingineili tuone ukubwa wa tatioz na kwa wilaya nyingine ilituweze kuchukua maamuzi ya dharura ya kumuomba Mbunge wetu kulisema kwa nguvu tatizo hili’’.
Kwa upande wake Mh. Jovitha Kombe, diwani wa Viti maalum, alitoa wito kwa waheshimiwa madiwani, mganga mkuu wa wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya kuweka utaratibu wa kuzitemebelea kaya ziilizopo wilayani Karagwe kwa lengo la kuzielimisha juu ya masuala ya lishe.
Kama ilivyo ada kwa mikutano mingine ya Baraza la Madiwani kutawaliwa na mjadala mkali kwenye ajenda zinazohusu masuala ya maji, vitambulisho vya taifa na sekta ya ujenzi wa barabara za mjini na vijiji, mkutano huu kwa mara nyingine ulikuwa na mjadala na mabishanao kati ya watendaji wa mamlaka hizo ambapo wajumbe wengi waliochangia katika ajenda hizo akiwemo Mh. Dawson Byamanyirohi na Mh. Magnus Cheus wa Kata ya Kibondo walionesha kutokuridhishwa na miradi ya maji katika kata za Rugera na Kibondo ambapo sababu ya kupasuka kwa mabomba katika maeneo hayo ilitajwa kama kikwazo kikubwa kinachokwamisha upatikanaji wa huduma hiyo kwenye maeneo hayo.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.