Na Innocent E. Mwalo.
Kikao cha Baraza la Madiwani kilifanyika hivi karibuni kwa muda kwa siku mbili, kikiwa pia ni kikao cha kwanza cha kazi tangu kuchaguliwa kwa Baraza jipya mnamo Novemba 2020, kimeazimia kwa kauli moja kuongezwaa kwa bidii na kubuniwa kwa mikakati mipya yenye lengo la kuongeza tija na kurahisha shughuli za maendeleo kwa wananchi wilayani hapa.
Awali katika hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mh.Wallace Mashanda, pamoja na kupongeza juhudi za menejimenti na uongozzi mzima wa wilaya hii katika suala nzima la ufaulu kwa shule za msingi na sekondari; huku akirejea matokea ya kidato cha nne kwa mwaka 2020 ambapo wilaya ya Karagwe imeshika nafasi ya tatu kati ya Halmashauri nane za mkoa wa Kagera, Mh. Mashanda alitoa maagizo anuai kwa wananchi na maenejimenti ya Halmashauri ya wilaya kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka 2021 wanaripoti shuleni mara moja. Agizo hili liilitokana na takwimu zilizoonesha kusuasua kuripoti kwa wanafunzi hao katika shule mbalimbali za serikali katika Halmashauri ya wilaya hii.
Aidha, katika kuliwekea mkazo suala la uimarishaji wa elimu wilayani hapa, Mh. Mashanda alitoa maagizo mengine kwa shule zote za msingi na sekondari wilayani hapa kuhakiksha kuwa wanafunzi wote wa shule hizo wanapata uji/chakula shuleni.
Agizo jingine la Mh. Mshanda lilikuwa ni juu ya upatikanaji wa takwimu sahihi za wananfunzi wanaokaa chini ili kuweza kuweka mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anayekaa chini.
Maagizo mengine yaliyopewa uzito katika hotuba ya Mh. Mashanda ilikuwa ni suala la maafisa ugani kubadilika hasa kwenye suala la usimamizi wa shughuli za kilimo kwa wakulima, pamoja na lile la kuhakisha suala la upimaji wa ardhi na makazi ya watu mijini na vijijini linawekwa kwenye mpango wa bajeti ili watu waweze kupata makazi bora pamoja na kuepuka migogoro ya ardhi inayoikumba wilaya hii kwa sasa.
Hali kadhalika, taarifa ya serikali iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mh. Godfrey Mheluka, ilijulisha na kuwaagiza wananchi wote kuchukua tahadhali zote muhimu kama vile kunawa mikono kwa maji tiririka, kutumia vitakasa mikono pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima kufuatia kuepuka kwa dalili za ugonjwa wa homa kali ya ‘’praenomina’’ ikiwa ni pamoja na homa kali, uchovu na kikohozi kikavu.
Kwa upande mwingine, Mhe. Mheluka alitoa taarifa kwa wananchi kupitia kikao hicho juu ya kuzuka kwa ugonjwa wa mafua ya nguruwe na ambapo katika jitihada za kuzuia maambukizi hayo kuenea, amepiga marufuku kwa muda, ulaji na usafirishaji wa nyama za nguruwe.
Aidha katika kujibu maswali yaliyoibuliwa na wajumbe wa kikao hicho ambao ni madiwani kutoka katika kata mbalimbali za wilaya, Mh. Mheluka aliagiza na kutoa ratiba ya siku tatu kwa ofisi yake kukutana na taasisi mbalimbali za serikali zilizopo wilayani hapa kwa ajili ya kushughulikia kero za maji, barabara, bei ya zao la kahawa, vitambulisho vya taifa pamoja na mambo mengine ambayo yaliibuliwa na kikwazo hiki kama masuala yanayokwaza juhudi za ustawi watu wa Karagwe.
Msisitizo mwingine uliotolewa na kikao hicho ulikuwa ni maazimio yaliyotokana na uwasilishwaji wa taarifa za wenyeviti wa Kamati tatu za kudumu za Halmashauri ya Wilaya yaani; Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango chini ya Mwenyekiti wake Mh. Wallace Mashanda, Kamati ya Elimu, Afya na Maji chini ya uenyekiti wa Mh. Charles Beichumila, na ile ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira inayoongozwa na Mh. Valence Kasumuni.
Kwa ujumla kikao hicho ambacho pia kilikuwa ni kikao cha robo ya pili kwa mwaka 2020/2021 kiliagiza na kuelekeza mambo kadhaa wa kadhaa kwa Idara za Fedha, Elimu, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Usafi na Mazingira ili kuboresha ustawi wa wananchi wa Wilaya ya Karagwe ikiwemo lile la Halmashauri kuongeza wigo wa kukusanya mapato kutoka vyanzo mbalimbali.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.