Leseni zinazotelewa na Halmashauri za Wilaya, Manispaa, Miji na Majiji ni za Kundi B. Leseni za Kundi A hutolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Mfano wa Biashara zilizo kwenye Kundi B:
Mwombaji anapaswa kujisajili katika mfumo wa ukusanyaji mapato wa Mamlaka za Serikali za Mitaa - TAUSI na kujaza kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha: -
(i) Jina la Biashara kama sio mtu binafsi (Certificate of Incorporation or Registration).
(ii) “Memorandum and Article of Association” kama ni Kampuni
(iii) Kitambulisho cha Taifa, Cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo kuonyesha kuwa ni Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Residnece Permit Class “A”).
(iv) Hati ya kiuwakili (Power of Attorney) kama wenye hisa wote wa Kampuni wapo nje ya nchi.
(v) Ushahidi wa maandishi kuwa una mahali pa, kufanyia biashara (Kwa mfano hati za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo au ardhi.
(vi) Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN).
Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali, Kwa mfano (TFDA, EWURA, TIRA, CRB, TILLI) n.k lazima mwombaji kuwa na cheti kutoka Mamlaka husika kabla ya kuomba leseni ya biashara.
NB: Leseni hii huisha muda wake mwaka mmoja (1) tangu tarehe ilipoanza kutumika.
Baada ya kujisajili na kuwasilisha maombi ya leseni yakiwa na viambatanisho sahihi, maombi hupitishwa ngazi zinazotakiwa kisheria – Mpango Miji, Mazingira, Afya na Biashara. Baada ya hapo leseni hutolewa ndani ya siku moja au mbili na si zaidi kupitia mfumo
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.