Shughuli za uvuvi hufanyika katika maziwa Burigi, Rwakajunju, Kamakala, Muguruka, Kaburi, Kitete, Chinyali na Mto Kagera pia kuna Mabwawa ya kuchimbwa na wananchi yapatayo 68 kwa ajili ya ufugaji wa Samaki.Uzalishaji wa samaki ni wastani wa kilo 343000.64 kwa Mwaka. Aina za Samaki wanaozalishwa kwa wingi ni Sato, Kambare Mambo (Kamongo), Kambare Mumi, Furu, Nembe, Domodomo, Kuyu na Dagaa. Wilaya yetu ya Karagwe ina Wavuvi takribani 340 na Wafanyabiashara wa samaki 110 ambao hufanya shughuli zao za kiuchumi kila siku ndani na nje ya Wilaya yetu. Karibu Wilayani Karagwe uwekeze kwenye vizimba vya ufugaji samaki, Mabwawa ya kuchibwa na uzalishaji wa vyakula vya Samaki.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.