Kituo cha Afya Kayanga chaongezewa milioni 100 kujenga wodi ya pili.
Na Geofrey A.Kazaula – Kayanga, Karagwe
Ujenzi wa Kituo cha Afya Kayanga umeongezewa nguvu baada ya Mh, Jenista Mhagama ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge Ajira na watu wenye ulemavu kutoa tamko la Serikali la kuongeza Shillingi Million Mia moja ( T.Sh 100,000,000.00) ili kuongeza jengo la wodi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa wodi ya akina mama unao endelea.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Kayanga , waziri Mhagama amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa huduma zinatolewa kwa wananchi na hasa wa hali ya chini kwa kuboresha miundombinu ikiwemo Sekta ya Afya.
Ameeleza kuwa miongoni mwa sababu za kufanya ziara katika Wilaya ya Karawe ni pamoja na kufuatilia maagizo mbalimbali ya viongozi na juu ya urejeshaji wa hali ya miundombinu baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi mnamo 10/09/2016.
Ameeleza kuwa kiu ya Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dk. John PombeJoseph Magufuli ni kuona huduma zinatolewa kwa wananchi na kueleza kuwa ujenzi wa wodi ya akina mama pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti ulio gharimu million 170.7 ukamilike mapema mwezi Oktoba/Novemba huu na kuanza kutoa huduma kwa wananchi .
Akiwa Kituoni hapo, Mh Waziri Mhagama alikagua shughuli za ujenzi zinazoendelea pia aliwatembelea akina mama waliojifungua pamoja na wagonjwa mbalimbali waliolazwa katika kituo cha afya Kayanga ambapo licha ya kuwapa pole alieleza kufurahishwa na kushuka kwa idadi ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua ikiwa ni baada ya kituo hicho kuanza kutoa huduma za upasuaji .
Kuhusu kinga dhidi ya njaa, Waziri Mhagama amewataka wananchi kulima mazao yanayo kabiliana na ukame badala ya kutegemea zao moja la ndizi kwaajili ya chakula na kusisitiza kuwa kila familia ilime mazao ya kinga ya njaa ili kujihakikishia juu ya upatikanaji wa chakula.
Amesisitiza juu ya matumizi mazuri ya fedha na kusema kuwa T.Sh 170,7 Milloni zilizoletwa na Serikali pamoja na T.Sh 100 Million itakayo letwa, fedha hizo zote zielekezwe katika kujenga wodi na kulitaka baraza la madiwani kusimamia fedha hizo ili zifanye kazi yenye tija itakayo wanufaisha wananchi.
Kazi ya ujenzi wa wodi ya akina mama na chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya Kayanga yenye thamani ya T.Sh 170.7 Milion ilianza mnamo tarehe 26/06/2017 na inatarajiwa kukamilika mnamo tarehe 6/10/2017 na Serikali imeridhia kuongeza kiasi cha T.Sh 100 Million kwa ajili wa ujenzi wa wodi nyingine.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.