MRADI WA ‘PS3’ WAANZA KUKUSANYA TAKWIMU KWA AJILI YA TATHMINI YA UTELEZAJI WA MRADI
Na Innocent E. Mwalo
Mradi unaojihusisha na shughuli za Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, wanakusudia kufanya kazi ya kukusanya Takwimu kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi huu kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
Mapema hivi karibuni, PS3 kwa kushirikiana na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa waliandaa mafunzo kwa Waratibu 16 wa Mradi huu kutoka katika Halmashauri zote nane zilizopo katika mkoa huu, mafunzo yaliyofanyikia katika Ukumbi wa Hotel ya ELCT iliyopo Mkoani humu ambapo lengo la mafunzo haya ilikuwa ni kuwajengea wataalam hawa uwezo kwenda kukusanya takwimu hizo.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo walikuwa ni ndugu Henry Shishira ambaye ni Meneja wa Mradi PS3 Mkoa wa Kagera, ndugu Fabian Gapchojiga ambaye ni Mwakilishi kutoka ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, ndugu Revocatus Mtesigwa ambaye ni mtaalam wa Mifumo kutoka PS3 Makao Makuu na Robert Mhongole ambaye ni Afisa TEHAMA wa Mradi wa PS3 Mkoani Kagera.
“Tumewaita hapa ili kuwajengea uelewa wa taarifa zinazopaswa kukuswa na kufanyiwa tathmini ambazo baadhi ya taarifa hizo bi pamoja na vipaumbele vya kijiji vilivyoingizwa kwenye mpango kazi wa Halmashauri, idadi ya wauguzi waliokuwa kazini na malalamiko yote yaliyorekodiwa kwenye rejista ya malalamiko kwa kipindi cha mwaka 2017/2018”, alisistiza ndugu Shishira katika ufunguzi wa mafunzo hayo.
Itakumbwa kwamba mradi Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) ambao utadumu kwa kipindi cha miaka mitano ulizinduliwa katika mwaka wa Fedha wa 2016/2017 na unafanya kazi kwenye maeneo matano ambayo ni Rasilimali watu, Mifumo ya kutolea taarifa, utawala bora, Fedha na eneo la utafiti.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.