WANANCHI WAASWA KUTUMIA MAJIKO BANIFU KUKABILIANA NA ATHALI ZA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE.
Katika hali ya kuwajengea uelewa wananchi wilayani Karagwe juu ya madhara ya matumizi makubwa ya mkaa na kuni na hivyo kupelekea ukatji hovyo wa misitu uongozi wilayani hapa uliweza kuwaalika kampuni ya LS Solution ambao ni watengenezaji wa majiko banifu kwa ajili kuhamasisha wananchi kununua majiko hayo ambayo yanatajwa kutumia kiasi kidogo sana cha nishati ya mkaa au kuni.
Uwepo wa matumizi makubwa ya mkaa upo katika maeneo kadhaa katika wilaya yetu ikiwemo miji yetu ya Kayanga na Omurushaka lakini pia miji ya Kihanga, Nyakaiga, Rwambaizi, Nyaishozi na Nyakasimbi.
“Hivyo basi kutokana na matumizi makubwa ya nishati ya mkaa katika nchi yetu, maadhimisho ya mazingira ya kitaifa yataongozwa na Kaulimbiu inayosema; “Mkaa Gharama; Tumia Nishati Mbadala”. Serikali imeweka Kaulimbiu hii kutokana na kiasi kikubwa cha maeneo ya misitu yanayoharibiwa kwa ajili ya kupata mkaa. Takwimu zinaonyesha kwamba mpaka mwaka 2017 kiasi cha hekta 46,942 huharibiwa kila mwaka”, alisisitiza Afisa Mazingira, Procesius Rweyendera.
Kwa maelezo ya Mlotwa Kasuku, ambae ni Naibu Masoko, wa Kampuni hiyo ya LS Solution, jiko hilo banifu lina sifa kadhaa ikiwemo kutumia aidha mkaa au kuni, lina bajeti nzuri ya mkaa au kuni, kutunza joto kwa muda mrefu, ni rafiki kwa mtu wa kipato cha chini na cha kati.
Sifa nyingine ni kwamba halitoi moshi wala kudondosha majivu na mwonekano wake hufanya taswira nzuri ya madhari ya maeneo ya jikoni.
Katika hatua nyingine, Meneja Masoko huyo alibainisha baadhi ya faida kuhusiana na matumizi ya jiko banifu ikiwemo kupunguza kasi ya ukataji wa miti kwa ajili ya uchomaji wa mkaa, kulinda uoto wa asili na viumbe hai.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.