Wananchi Karagwe Waanza kunufaika na mradi wa umwagiliaji.
Na Geofrey A.Kazaula
Mradi wa umwagiliaji unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe maarufu kama’Mwisa Irrigation Scheme’sasa umeanza kuwanufaisha wakulima kwa kuwa na kilimo cha uhakika cha umwagiliaji.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bujuruga wakati wa kukabidhi mradi huo kwa kamati ya usimammizi, Mh, Diwani wa Kata ya Bugene Aristides Muliro amehamasisha juu ya kilimo cha umwagiliaji na hasa kilimo cha mpunga.
Kwa upande wao, wananchi wa kijiji cha Bujuruga ambao ni wanufaika wa kwanza wa mradi huo, wameeleza furaha yao ya kukabidhiwa mradi huo ambao sasa unatumika, wanalima na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.
Bwana Faridu Ahmada ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Bujuruga ambaye alieleza kufurahishwa na Jitihada za Serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi hasa kwa upande wa kilimo.
‘Wananchi wa Bujuruga na maeneo ya jirani kwa sasa wana kilimo cha uhakika kutokana na mradi huu wa umwagiliaji kwani hakuna haja ya kusubiri mvua na sasa tunaona matunda mazuri ya Serikali ya awamu ya tano katika kuwajali wananchi wake’ alisema Mwenyekiti huyo.
Ili kuendelea kuwa na maji ya uhakika katika mradi huo, Wakala wa huduma za Misitu ( TFS) wameendelea kuboresha mazingira kwa kugawa mbegu za miti kwa wakulima wa Karagwe ili kuhifadhi mazingira.
Kwa mujibu wa Bwana Sunday J. Anut ambaye ni meneja wa misitu TFS, kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira katika Wilaya ya Karagwe ili kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
‘TFS tunaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kugawa mbegu za miti kwasababu tuna amini hata mradi huu utaendelea kupata maji ya kutosha kama uhifadhi wa mazingira utazingatiwa’ alisema Meneja huyo wa TFS Karagwe.
Hadi sasa baadhi ya Kata zimenufaika na huduma za Wakala wa Misitu kwa kupatiwa mbegu za miti na elimu ya uhifadhi wa mazingira ambapo taasisi za umma na watu binafsi pia wamepatiwa mbegu za miti.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.