Na Geofrey A. Kazaula
Wa taalam kutoka Benki Kuu ya Tanzania ( BoT) wametoa elimu kwa wananchi Katika Wilaya ya Karagwe juu ya namna Benki hiyo inavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na fursa zilizopo katika Benki hiyo ambapo wananchi wanaweza kukuza kipato chao kwa kushiriki kununua dhamana za Serikali.
Kwa mujibu wa wataalam hao, Kuanzia Mei 2, 2014, Tanzania iliondoa vikwazo kwenye uwekezaji katika masoko ya dhamana za serikali na dhamana za mitaji kwa wakazi wote wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Kupitia mabadiliko ya kanuni za kubadilisha fedha za kigeni (Foreign Exchange listed securities Regulations of 2003 and Foreign Exchange Regulations of 1998).
Kutokana na hali hiyo sasa wananchi wameshauriwa kuwa wanaweza kufanya uwekezaji wenye tija na uliosalama kwa kununua dhamana za Serikali za muda mfupi na za muda mrefu ili kuiwezesha Serikali kugharamia makisio katika bajeti yake katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa pale Serikali inapokuwa imepungukiwa fedha kulingana na matumizi ya kipindi husika.
Akizungumza na wafanyabiashara, viongozi na wataalam mbalimbali katika Mji wa biashara ‘Omurushaka’, Mchambuzi wa masuala ya fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania Ndg, Fidelis B.Mkatte amefafanua kuwa kwa kununua dhamana za Serikali, wananchi hupata fursa ya kuikopesha Serikali na kuiwezesha kutekeleza majukumu yake na kisha kumrejeshea mhusika fedha yenye riba kubwa na ya uhakika kwa wakati.
‘‘ Naomba ni watoe wasiwasi wananchi wote kuwa uwekezaji uliosalama ni kununua dhamana za Serikali na hili linawezekana kwa kila mtu mwenye mtaji wa kuanzia T.Sh 500,000 ( Laki tano tu) hivyo si sahihi kabisa kuamini kuwa suala hili ni la wafanya biashara wakubwa tu’’ alisema mtaalam huyo.
Kwaupande wake Afisa Mahusiano wa Benki Kuu ya Tanzania Ndg, Victoria J.Msina amewasisitiza wananchi kuwa Sehemu sahihi ya kufanya uwekezaji ni kununua dhamana za Serikali kwani uwekezaji huo ni wa uhakika na Serikali inalinda wateja wake kuliko mashirika binafsi na taasisi binafsi za kifedha.
‘‘ Benki kuu ni chombo cha Serikali na Serikali ina uhakika wa kutoa riba za mwananchi kwa wakati pia mikataba ya Serikali ina uhakika na faida kubwa kuliko Benki za biashara hivyo na wasihi kuwekeza katika Serikali kwani pia kwa kufanya hivyo tunaiwezesha Serikali kutekeleza miradi yake kwa wakati’’ alisema mtaalam huyo.
Elimu hiyo pia imetolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mkutano wa hadhara na kikao kilicho wahusisha wataalam wa Halmashauri, wafanyabiashara na wa heshimiwa madiwani ambapo pamoja na mambo mengine wananchi wamefundishwa namna ya kuitambua fedha halali ya Tanzania na namna ya kuhifadhi fedha.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.