WALIMU WA AFYA WAAGIZWA KUSIMAMIA USAFI WA VYOO MASHULENI
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE
Kamati ya Huduma za Afya, PHC kwa kauli moja wamewaka azimio kwa walimu wa afya na wadau wengine katika sekta ya Afya, Elimu na Utawala kuzisimamia taasisi zao katika kuhakikisha ya kwamba suala la usafi wa vyoo linatiliwa mkazo ili jamii ya wanafunzi na wananchi katika maeneo hayo iweze kuona umuhimu kuzingatia suala hilo la usafi.
Azimio hilo lilifikiwa katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi hivi karibuni chini ya Mkuu wa Wilaya ya Karagwe ambapo mara hii Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa Katibu Tawala Wilaya, Mh. Innocent Nsena ambapo azimio hili lilikuja kutokana na taarifa iliyowasilishwa katika kikao hicho ikionesha ya kwamba hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu, wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wameshajenga vyoo kwa asilimia 65.3
“Tunaagiza Idara ya Afya, Elimu na Utawala kuhakikisha mnazisimamia vema taasisi zenu zinazotoa huduma katika maeneo yetu ili kuhakikisha suala la usafi linawekewa mkazo na hiyo ni kutokana na kukithiri kwa uchafu kwa baadhi ya taasisi hasa shule hali inayoweza kupelekea kutokea kwa mlipuko wa magonjwa hasa katika msimu wa mvua”, alisisitiza mmoja wa wajumbe katika kikao hicho.
Aidha kikao hicho ambacho hufanyika kila robo isipokuwa kama kutakuwa na dharura kiliweza kujadili taarifa mbalimbali ikiwemo zile zinazohusu Utoaji wa Huduma za Chanjo, taarifa ya kampeni ya Dawa ya Kichocho na Minyonyo, taarifa ya CHF iliyoboresha.
Katika kujadili baadhi ajenda hizo wajumbe waliweka msisitizo mwingine katika suala la kuhamasisha jamii katika mpango wa serikali wa kumezesha dawa ya kichocho na minyoo kwa wanafunzi wa shule za msingi wenye umri wa miaka 0- 15 jambo litakalotekelezwa kuanzia Juni 25, 2018 hadi Julai 13, 2018.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.