‘WANANCHI LIMENI AINA YEYOTE YA MAHARAGE KADRI MNAWEZA KUPATA SOKO’ – KAMATI YA UJENZI, UCHUMI NA MAZINGIRA
Na Innocent E. Karagwe, KARAGWE.
Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, chini ya Mwenyekiti wake Mh. Valence Kasumuni kwa kauli moja, kupitia kikao chake kilichoketi hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri, Wilayani hapa, wameazima wananchi wa Karagwe waendelee kulima aina yeyote ya maharage kadri wanavyoona wanaweza kupata uhakika wa masoko kwa ajili ya kuyauza.
Uamuzi huu ulifikiwa ili kuzima uvumi unaoeneo katika baadhi ya maeneo wilayani hapa ukidai kwamba serikali imewazuia wakulima wa zao la maharage kulima aina fulani ya maharage hayo huku na ukilazimisha kulimwa kwa aina fulani ya maharage jambo ambalo si kweli kwa mujibu wa taarifa za kikao hicho.
Katika hatua nyingine kikao hicho kilipokea na kujadili taarifa nyingine zilizozihusu Idara na Vitengo kadhaa ambavyo kwa mujibu wa sheria huwasilisha taarifa zao kwenye kamati hiyo.
Idara hizo zilikuwa ni pamoja na Idara ya Ujenzi, Usafi na Mazingira, Idara ya Ardhi na Maliasili na Kitengo cha Ufugaji Nyuki.
Aidha taarifa za Idara za Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, Mifugo na Uvuvi na Kitengo cha TEHAMA ziliweza kuwasilishwa kupitia kikao hicho.
“Tunaendelea kusisitiza kwamba Idara ya Ardhi na Maliasili ishirikishe makampuni binafsi katika upimaji wa ardhi wilaya Karagwe ili kuweza kuongea kasi ya upimaji ” walisisitiza wajumbe katika mjadala wao kwenye mojawapo ya ajenda zilizowasilishwa kikaoni hapo.
Aidha msisitizo mwingine kwenye kikao hicho ulikuwa ni juu ya wananchi kusisitizwa juu ya azma ya serikali katika mikakati ya kuboresha zao la kahawa na hii ni kutokana na serikali kuweka mkazo katika zao hilo la biashara ambapo wananchi wanapaswa kujengewa uelewa wa kuzingatia uuzaji wa zao hilo kwenye vyama vya msingi ambapo hadi sasa maafisa ushirika wanaendelea kutoa Elimu ya ushirika kwa wananchi wa maeneo hayo.
Vikao vingine vya kamati vinatarajiwa kuendelea ili kufanikisha kufanyika kwa kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani hapa kinachotarajiwa kufanyika mnamo Mei 18- 19, mwaka huu.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.