Na, Geofrey A .Kazaula
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe inaendelea na zoezi la chanjo ya ng’ombe ili kutoa kinga kwa magonjwa ya Chambavu na Kimeta.
Chanjo ya mifugo inayoendelea inaendeshwa kwa mujibu wa sheria Namba 17 ya kuzuia magonjwa ya mifugo ya mwaka 2003 .
Wafugaji wote katika Kata zote 23 wamefahamishwa kuwa wana wajibu wa kushiriki kikamilifu zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuleta mifugo yote kulingana na ratiba ya chanjo iliyotolewa kwa kila Kata na Vitalu vya wafugaji.
Aidha zoezi hili la chanjo litahusisha kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote watakao kiuka ama watakaoficha mifugo ama kugoma kabisa kushiriki.
Kwamujibu wa Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Ndg, Kulwa J. Mkwama, ratiba ya chanjo itafatwa kama ilivyopangwa kwa kila eneo na kwa Kata zote 23 za Wilaya ya Karagwe na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakao bainika kukaidi ama kukwamisha zoezi hilo.
‘‘ Nitumie nafasi hii kuwafahamisha wananchi wote kuwa zoezi la chanjo linalo endelea lipo kwa mujibu wa Sheria na yeyote atakaye bainika kukwamisha zoezi hili la chanjo ya mifugo atachukuliwa hatua za kisheria mara moja hivyo wafugaji wote wanapaswa kushiriki kikamilifu’’ . alisema Mtaalam huyo.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Ndg, Godwin M.Kitonka ameeleza kuwa Halmashauri imejipanga kusimamia kikamilifu zoezi hili la chanjo na kwamba atahakikisha zoezi linasimamiwa vizuri kwa Kata zote 23 ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wtakao bainika kukwamisha zoezi hilo.
‘‘ Sisi kama Halmashauri tumejipanga vizuri ili kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wafugaji wetu lengo likiwa ni kutoa kinga ya magonjwa kwa mifugo na pia hatutasita kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakaye bainika kukwamisha zoezi hili’’ alisema kiongozi huyo.
Zoezi la chanjo kwa sasa linaendelea katika Kata ya Kihanga,Nyakasimbi na Rugu ambapo linahusisha wafugaji wote pamoja na Vitalu vya wafugaji na lina tarajia kukamilika mnamo mwezi wa tatu 2019.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.