VIONGOZI WILAYANI KARAGWE KUFANYA KAMPENI YA AFYA
Na Frank I. Ruhinda, KARAGWE.
Viongozi wakuu Wilayani hapa wameanza kutekeleza kwa vitendo agizo lillofikiwa kwenye kikao cha Afya ya Huduma ya Msingi (PHC) kilichofanyika mnamo tarehe 23/08/2018 katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Katika kikao hicho wajumbe kwa kauli moja waliazimia uongozi wa wilaya kufika kwenye maeneo yote ya utawala yaliyopo wilayani hapa kwa ajili ya kufanya kampeni mbalimbali za afya zenye lengo la kuboresha afya ya jamii kwenye maeneo hayo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ndugu Godwin M. Kitonka ambapo ameyataja maeneo hayo ambayo kampeni hiyo itafanyika ikiwemo eneo la Nyakaiga katika Kata ya Kibondo likihusisha tarafa za Nyabiyonza na Nyakakika mnamo tarehe 12/09/2018.
Aidha kampeni hiyo inatarajiwa kuendelea mnamo tarehe 13/09/2018 kwenye eneo la Rwambaizi katika Tarafa ya Kituntu, Tarafa ya Bugene na Tarafa ya Nyaishozi.
Katika kampeni hiyo yenye lengo la kuhamasisha jamii juu ya kuzingatia chanjo zote zinatolewa na Idara ya Afya, kuhamasisha akina mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma, kuhamasisha jamii juu ya ujenzi na matumizi bora ya vyoo pamoja na kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya vyandarua viongozi wakuu katika wilaya ambao ni Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji wakiambatana na wataalam mbalimbali kutoka Idara ya Afya watafika kwenye maeneo hayo kwa ajili ya bshughuli hiyo.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.