USAILI WAFANYIKA KWA WATUMISHI WA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE.
Kikao cha Bodi ya Ajira katika Halmashauri ya Wilaya Karagwe, kimeendesha zoezi la usaili kwa waombaji wa kada ya watendaji wa vijiji daraja la tatu ambapo jumla ya waombaji wapatao 225 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi la usaili wa kuandika kabla ya mchujo na kisha kubakiwa na watu wachache wenye vigezo kwa mujibu wa matokeo ya mtihani huo watakaoendelea na mchujo wa ana kwa ana/ mahojiano.
Mapema Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala katika Halmashauri hii alisikika akizungumza na washiriki hao ambapo pamoja na mambo mengine amewasisitiza kuzingatia kanuni na tratibu zote katika zoezi hilo kwa kuepuka kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo kwani kufanya hivyo kutakuwa ni kukiuka taratibu na sheria.
“Nawasihi sana kila mmoja wenu awe mwaminifu katika zoezi hili na naamini kila mmoja wenu amejiandaa vizuri na niwatakie kila la heri”, Mwakisu aliwaambia washirika hao.
Zoezi hili la usaili kwa watumishi wa kada hii linafanyika kufuatia kibali kilichotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti, Sekretariei ya Utumishi wa Umma kufuatia upungufu wa watumishi wa kada hii.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa waombaji wa kazi hii na elimu ya kidato cha nne au cha sita na mafunzo ya astashahada au cheti katika moja ya fani ikiwemo utawala, sheria, Elimu ya Jamii, usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na sayansi ya Jamii.
Pamoja na mambo mengine watendaji hawa watapaswa kutimiza majukumu yafuatayo:- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji, kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao na kukusanya mapato ya Halmashauri.
Majukumu mengine ni kama vile kusimamia, kukusanya, kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za vijiji, kuwa katibu wa mikutano ya Halmashauri ya Wilaya, kusimamia utungaji wa sheria ndogo za vijiji, kuwa afisa masuuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji pamoja na kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.