Na, Geofrey Archard Kazaula
Wananchi Wilayani Karagwe wame endelea kupatiwa elimu juu ya kutokomeza uvuvi haramu kwa lengo la kuwa na uvuvi endelevu usio kiuka sheria.
Akizungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali inakofanyika biashara ya samaki, Afisa Uvuvi Wilayani Karagwe ndg, Siima Kazoba amefafanua kuwa uvuvi haramu usipo pigwa vita utapelekea kumalizika kabisa kwa samaki na mazao ya majini kama dagaa na mengine.
Ame eleza kuwa uvuvi haramu ni pamoja na kuvua samaki wachanga wasio kidhi vigezo vya kisheria, kuvua kwa kutumia makokoro, na njia nyingine za uvuvi ambazo zinakinzana na sheria.
Ili kumaliza tatizo la uvuvi haramu, Wilaya kupitia Sekta ya Uvuvi ime endelea kutoa elimu kwa umma hasa katika Kata za Rugu, Bweranyange na Kamagambo ambapo kwa kiasi kikubwa biashara ya samaki hufanyika.
Akifafanua juu ya Elimu inayotolewa kwa wananchi, Afisa huyo ame eleza kuwa wananchi wanapatiwa elimu juu ya kusajiri mitumbwi, kulipia leseni za mitumbwi, kuvua samaki wanao kidhi vigezo,kulipia leseni za biashara ya samaki na mazao ya majini, na kutoa elimu juu ya athari za uvuvi haramu kwa mapana yake.
‘‘ Kwanza tumejikita mno katika kutoa elimu kwa wanachi kabla ya kuwatoza faini ili tunapo mkamata mtu anayekiuka maelekezo yaliyotolewa aelewe kabisa kuwa atatozwa faini kwa mujibu wa sheria.’’alisema Afisa huyo.
Kutokana na elimu inayo endelea kutolewa, wananchi wameanza kufanya biashara ya samaki kwa kufuata sheria na kanuni na lengo la Wilaya ni kuhakikisha Uvuvi haramu unatokomezwa kabisa na kufikia hatua ya kila mwananchi kufanya biashara ya samaki pamoja na mazao ya majini kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.