Timu ya Mkoa yakagua Miradi ya Mwenge wa Uhuru 2017 Wilayani Karagwe
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE.
Timu ya mkoa imefanya ukaguzi wa miradi itakayowekewa jiwe la msingi na ile itakayozinduliwa wakati mwenge wa uhuru 2017 utakapowasili Agosti 03, 2017 wilayani humu.
Ugeni huo toka mkoani ulioongozwa na ndugu Said Mustapha uliwasili wilayani hapa Karagwe tarehe 17/06/2017 na kupokelewa na Bi. Nyangele Makunenga, Kaimu Katibu Wilaya wa wilaya akishirikiana na Bi. Ashura Kajuna, Kaimu Mkurugenzi wa wilaya aliyekuwa ameambatana na timu ya wataalam toka Halmashauri na walianza kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa wodi ya wanaume katika kituo cha afya Kayanga.
Mradi huu wenye thamani ya milioni 170,000,000 unatarajiwa kuwekewa jiwe la msingi na mwenge wa uhuru na kwa mujibu wa Mganga Mkuu wilaya, Dkt. Libamba Sobo ujenzi wake utaanza mapema ili ifikapo ratiba ya mwenge uwe umefika hatua fulani ya ujenzi.
Msafara ulinza kwa kutembelea mradi wa kiwanda cha kumenya kahawa mbivu cha KADERES kilichopo kata ya Ndama ambapo uzinduzi wa kiwanda kinachokadiwa kujengwa na mmiliki wa kiwanda hicho kwa thamani ya milioni 253,000,000 unatarajiwa kufanywa na mbio za mwenge 2017.
Mradi mwingine uonayotarajiwa kuzinduliwa na Mwenge huu wa uhuru ambapo timu ya mkoa ilitembea ilikuwa ni ujenzi wa mabweni mawili ya wavulana katika Shule ya Sekondari Bugene, mradi unakadiriwa kugharimu takribani milioni 162,000,000 ikiwa ni mchango toka kwa wahisani na kiasi kingine kikitolewa na Halmashauri ya wilaya.
Mradi mwingine uliotembewa ulikuwa ni kikundi cha vijana selemara cha Kayanga ambapo kikundi hiki kinatajiwa kukabidhiwa hundi na kiongozi wa mbio za mwenge.
Kikundi cha wanawake MVIKAKATI- KITUNTU pia kimo katika orodha ya kukabidhiwa hundi katika ratiba ya mwenge wa uhuru mwaka huu.
Mradi mwingine ambao jiwe la msingi litawekwa ni mradi wa maji mjini uliopo Kata ya Bugene eneo la kishao kwenye kijiji cha Rukajange. Huu ni mradi unaotajwa kugharimu kiasi cha 1,890,000,000 ikiwa ni fedha toka serikali kuu.
Baada ya timu hii kutoka mkoani kuelekea wilayani Kyelwa, timu yaw a wataalam toka Halmashauri ya wilaya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama waliendelea kutembelea miradi mingine ya kilimo, uvuvi na ufugaji ambapo ujumbe huu ulitembea bwawa la kufugia samaki katika kijiji cha Rukale kata ya Nyaishozi linalomilikiwa na kikundi cha CHAVUMA chini ya uenyekiti wa Boaz Katoke.
Mradi mwingine ambao unapendekezwa kuwekwa kwenye ratiba ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni ule wa shamba la miti linalomilikiwa na ndugu Jackson Iganiza, shamba linalokadiriwa kuwa na miti 4950.
Mradi mwingine unaopendekezwa kuzinduliwa ni daraja(box culvert) linalojengwa kwenye barabara ya Kajunguti -Rubale -Misha. Mradi huu unakadiriwa kujengwa kwa takribani milioni 15,598,000 ikiwa ni fedha kutoka mfuko wa barabara.
Klabu ya wapinga rushwa iliyopo katika Shule ya Sekondari Nyakasimbi ni mojawapo wa miradi itakayozinduliwa katika ratiba hii ya mwenge wa uhuru.
Kama miradi hii itakubaliwa na kikao cha mwenge cha wilaya kuna uwekano mkubwa wilaya hii kufanya vizuri zaidi katika mwenge wa uhuru mwaka huu kwani miradi ya Elimu, Afya, Barabara, Maji, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ni moja ya miradi inayoainishwa kuwa na alama kubwa katika tathmini ya mwenge wa uhuru 2017. Itakumbukwa kuwa mwaka 2016 wilaya ya Karagwe ilishika nafasi ya nne kati ya Halamashauri nane za mkoa wa Kagera.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.