Timu ya Mkoa Yafanya Ukaguzi wa Miradi ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2018 Wilayani Hapa.
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE.
Timu ya watu watano (05) kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera imefika wilayani hapa na kukagua miradi inayotarajiwa kuzinduliwa na mbio za mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwepo wilayani hapa mnamo Aprili 13, 2018.
Ujumbe huo ulioongozwa na ndugu Ernest Matala ambaye alikuwa emeambatana na ndugu Geneveva Emmanuel, ndugu Projestus Kato, ndugu Mmayya Mbaraka na ndugu Twalib Ramadhani ambao ni wajumbe wa Kamati ndogo ya mwenge wa mkoa ambapo ujumbe huo uliambatana na Timu ya wilaya iliyokuwa ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Mh. Nyangele Makunenge aliyekuwa ameambatana na wajumbe wengine wa Kamati ya Mwenge ya Wilaya ambao ni ndugu Romanus Msafiri, ndugu Peter Mmbare, ndugu Mmasa Mmasa na ndugu Aloyce Mujungu.
Timu hii ilifanya ukaguzi wa miradi yote pendekezwa kwa ajili ya mbio za mwenge wa Uhuru 2018 ambayo ni Klabu ya Wapinga Rushwa iliyopo shule ya Sekondari ya Rwambaizi, ujenzi wa vyumba vya madarasa vitatu (03) na ofisi moja ya walimu, vyoo na matundu 11 na kisima cha maji katika shule ya Msingi Omurwere Rwambaizi.
Miradi mingine ni shamba la migomba la ndugu Mtawajibu Kajoki, kiwanda cha kusaga na kusindika unga wa mahindi cha Karim Amri, barabara za lami mjini Kayanga, wodi za kituo cha afya Kayanga na kikundi cha wanawake NDAWOSA.
Miradi mingine ambayo ujumbe huo ulizuru ilikuwa ni mabanda ya UKIMWI, Malaria, kupinga rushwa na madawa ya kulevya ambayo kwa ujumla inatajwa kuwa miradi ya kiasi 6,573,400,000.00 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Mwenge Wilayani hapa ndugu Mmasa Mmasa.
“Tumetembelea miradi hii na tunapongeza maandalizi yaliyokwisha kufanyika mpaka sasa lakini tunatoa wito wa kufanya marekebisho kadhaa ikiwemo kufyekwa kwa barabara ya Rwambaizi – Omurwere na kufikiria kitu cha tofauti kwenye miradi ya Klabu ya wapinga rushwa na kwa upande wa wodi
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.