TANGAZO KWA WANANCHI WOTE WANAOJISHUGHULISHA NA UVUVI NA BIASHARA YA SAMAKI NA MAZAO YATOKANAYO NA UVUVI
Kwa mujibu wa sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 pamoja na kanuni za uvuvi za mwaka 2009
mnakumbushwa kulipia ada za leseni za kukusanya, kusafirisha na kuuza samaki pamoja
na leseni za mitumbwi kwa mwaka 2017 na mwisho wa kulipia kwa hiari ni tarehe 30/4/2017
Ni marufuku kwa mtu yeyote kujihusisha na uvuvi pamoja na ukusanyaji wa mazao yatokanayo na uvuvi
bila kua na vibali halali kutoka ofisi za uvuvi
Wasafirishaji na wachuuzi wa samaki kutoka nje ya wilaya hii, hakikisheni samaki wanaoingizwa wanaambatana na vibali vya usafirishaji samaki kutoka sehemu husika.
IMETOLEWA NA
GODWIN M. KITONKA
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.