Sita Mbaroni kwa Uvuvi Haramu Wilayani Karagwe
Na , Geofrey A. Kazaula Afisa Habari Karagwe
Watuhumiwa sita wamekamatwa wakijihusisha na shughuli za uvuvi haramu katika ziwa Burigi Wilayani Karagwe.
Wavuvi hao walikamatwa wakiwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia shughuli hiyo ikiwa ni pamoja na Kokoro lenye thamani ya Shillingi Millioni nne.
Kwa mujibu wa Afisa uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe bwn, Remigius Christian, uvuvi haramu una athari kubwa sana ikiwa ni pamoja na kusababisha uharibifu wa mazingira, kuharibu mazaria ya samaki, kuua viumbe hai wa majini na hatimaye kusababisha kupungua au kutoweka kwa samaki .
Wakitoa maelezo ya awali, wavvuvi hao walieleza kuwa biashara hiyo wanaifanya wakiwa wametumwa na mwajiri wao kutoka Wilaya jirani ya Muleba.
Kwaupande wake Diwani wa kata ya Rugu Mh, Adrian Kobushoke amewataka wananchi kuenndelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uharifu wa aina hiyo na kwamba kwa kufanya hivyo watadhibiti uvuvi haramu na kujipatia kitoweo cha kutosha kila siku ikiwa ni pamoja na kujipatia mapato kutokana na biashara ya samaki.
Hadi sasa watuhumiwa wote sita wanashikiriwa na jeshi la polisi na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.