Rais Magufuli amwaga neema ya vitanda Kituo cha Afya Kayanga
Na Innocent E. Mwalo, Karagwe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo tarehe 09/08/2017 ametoa zawadi ya vitanda 20 kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa kwenye kituo cha Afya cha Kayanga ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati akiwa kwenye kampeni za kuwania kiti cha uraisi mwezi Septemba 2015 wilayani hapa.
Akikakabidhi vitanda hivyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, mbunge wa Jimbo la Karagwe Mh. Innocent Lugha Bashungwa amemmwagia sifa kemkem Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutimiza ahadi yake hiyo ya kutoa vitanda vitakavyotumiwa na wananchi wanyonye watibiwapo kwenye kituo hicho cha Afya.
Vitanda hivyo vinatarajiwa kupunguza adha ya wagonjwa kulala chini wawapo katika matibabu kituoni hapo.
Huku akitoa wito kwa uongozi wa Wilaya na Kituo hicho cha Afya kuvitunza vitanda hivyo, Mh. Bashungwa amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja anayehusika kuvitunza vitanda kwani ni matarajio ya serikali ni kuona vimadumu kwa muda mrefu.
“Nakuomba Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya, Mkuu wa Kituo hiki cha Afya, na wauguzi kuhakikisha vitanda hizi vinatunzwa ili siku Rais Magufuli akija avikute vitanda hivi vikiwa katika hali nzuri”, alisisitiza Mh. Bashungwa huku akishangiliwa na wananchi walikusanyika kumsikiliza.
Akipokea vitanda hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya Karagwe ameishukuru serikali ya Rais Magufuli kwa mambo mengi inayowatendea wananchi wa Wilaya ya Karagwe hasa upanuzi wa Kituo cha Afya Kayanga unaendelea na kuahidi kwamba vitanda hivyo vitatumika kama ambavyo serikali imeagiza.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.