PROFESA KAMUZORA AWA DARASA KATIKA SHUGHULI ZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA WILAYANI KARAGWE.
Na Innocent E. Mwalo.
Katika Jitihada za kuunga mkono shughuli za Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira, Mhadhiri kutoka Chuo kiku cha Mzumbe, Profesa Auleria Kamzora amefika na ujumbe kutoka Chuo Kikuu hicho kwa lengo la kufanya mambo kadhaa yenye lengo la kuhamasisha jamii ya Karagwe juu ya utunzaji wa mazingira.
Katika kutekeleza azima hii, Profesa Auleria hizi karibuni aliweza kuwaleta wageni na wanafunzi ambao ni wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe ambao anashirikiana nao katika kuratibu Programu Shirikishi kati ya Afrika, Ulaya na Asia.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Kata ya Kituntu yalionekana kumshawishi zaidi Profesa Auleria katika kufadhili juhudi za uhifadhi wa mazingira zinazotekelezwa wilayani hapa.
“Aidha, binafsi na kwa niaba ya wananchi Wilayani hapa, tunawapongeza sana wahitimu hawa kwa kuhitimu masomo ya Chuo Kikuu Mzumbe”, alisema Mh. Wallace Mashanda, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hii.
Huku akinukuu nadharia mbalimbali za wanazuoni, Mh. Mashanda aliweza kuainisha ya kwamba Jina “ Karagwe “ kutokana na simulizi za wazee wetu mbali mbali na watafiti wa historia ya Karagwe kama ( Katoke 1975; 162) inaelezwa kwamba jina hili linatokana na kilima kinachopatikana Kusini Magharibi ya Makao makuu ya wilaya ya Karagwe ,kwenye kijiji cha Kandegesho ,kata ya Nyakakika ambacho mtawala ( Omukama ) wa kwanza alifanya kafara ya kwanza.
Kwa mujibu wa Mh. Mashanda alieleza kuwa kwa mujibu wa taarifa zilizopo mtawala huyo alijulikana kwa jina la Nono ya Malija kutoka ukoo wa Basiita. Na kwamba kumbukumbu hii ya “Karagwe ka Nono “inatokana na ukweli kuwa Nono alikuwa mtawala wa mwisho wa wenyeji asilia kabla ya kuondolewa madarakani na Omukama Ruhinda mtoto wa Wamara. Inasemekana kwamba Nono aliondolewa kwa ujanja bila ya misukosuko wala mapigano ya aina yoyote. Kwa kifupi hii ndio kumbukumbu yake na chimbuko la historia ya jina Karagwe
“Kwa ujumla Hali ya upatikanaji wa chakula katika wilaya ni nzuri. Mazao yanayolimwa ni ya kudumu kama vile ndizi na kahawa, na mazao ya muda ni maharage, mahindi, viazi mviringo, viazi vitamu, viazi vikuu, mihogo, njegere, mtama,ulezi,njugumawe, kunde, alizeti, magimbi na karanga. Pia kuna mazao yasiyolimwa wilayani ambayo yanapatikana sokoni na kwenye magulio ya kata na vijiji, mazao hayo ni mchele na ngano ambayo yanapatikana kwa bei nafuu”, alibainisha Mh. Mashanda kupitia hadhara hiyo.
Zao la biashara wilayani hapa ni kahawa huku ndizi na maharage yakiwa ni mazao ya chakula na biashara.Shughuli nyingine za uzalisahi mali ni ufugaji na uvuvi.
Kuhusu Sekta ya Utalii, Mh . Mashanda aliweza kubainisha kupitia hotoba yake ya kwamba Wilaya ya Karagwe ina mbuga ya wanyama ya Chato ambayo imeundwa Mapori mawili ya Akiba ya wanyamapori ambayo ni Kimisi na Burigi. Mbuga hii ina wanyama wengi Kama vile pofu, nyemera, mamba, viboko, twiga, simba, kuro, nyati, tembo na ndege wa aina wa aina mbalimbali.
Mbuga hii mbali na kuwa kivutio kwa watalii na wananchi wanaopenda kuangalia wanyamapori, mito na mabonde; vile vile hutumika kwa shughuli za utalii wa picha.
“Kivutio kingine ni mapango ya Kituntu, kijiji cha Kijumbura kwenye kata ya Bweranyange yalipokuwa makao makuu ya mukama Rumanyika. Aidha kuna mti wa mwembe uliopo katika Kijiji cha Kafuro Kata ya Nyabiyonza ukiopandwa na kuachwa na waarabu mnamo karne ya 18, ziwa Kitete lenye wanyama aina ya kiboko wengi”, alibainisha Mh. Mashanda.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.