Naibu Waziri aacha Maigizo Wilayani Karagwe
NA Innocent E. Mwalo, KARAGWE
Naibu Waziri Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Suleimani Jafo, amefanya ziara ya kikazi Wilayani Karagwe mnamo 25Julai, 2017 huku akikagua na kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo wilayani hapa ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano na wananchi katika maeneo kadhaa kadhalika kuongea na watumishi katika ukumbi wa Angaza.
Naibu Waziri Jafo aliwasili katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Karagwe na kulakiwa na Mkuu wa Wilaya hii Mh. Godfrey Ayoub Mheluka, Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe ndugu Godwin M.Kitonka aliyekuwa ameambatana na wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na baadhi ya watumishi wa Halmasahuri ya Wilaya Karagwe.
Ziara yake ilianzia katika kitua cha Afya Kayanga ambapo Naibu Waziri Jafo alipata kujionea ujenzi wa wodi ya wanaume unaondelea katika maeneo hayo unaojengwa kwa kiasi cha fedha cha takribani milioni 170 ikiwa nifedha kutoka Serikali kuu.
Katika eneo hili, kiongozi huyo alipata wasaa wa kukuagua pia maabara inayojengwa katika kituo cha Afya hiki huku akibain mapungufu kadhaa ikiwemo kukosekana kwa mabomba ya maji katika baadhi ya vyumba ambapo alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe, ndugu Godwin M. Kitonka kuhakikisha anasimamia kila chumba kinajengewa mabomba ya maji kwa ajili ya huduma ya maabara.
Mh. Jafo alizuru eneo la Nyakayanja, kata ya Nyaishozi mahala ambapo kinajengwa kituo kingine cha afya ambacho pindi ujenzi wake utakapokamilika utapunguza msongamano wa utoaji wa Huduma kwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Nyakahanga pamoja na kituo cha Afya cha Kayanga.
Katika eneo hili Mh. Jafo alitoa maigizo kadhaa kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe ikwemo kuhakikisha milioni saba zinazohitaji kwa ajili ya mfumo wa umeme zinapatikana.
Pia alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hii, kuhakikisha kwamba mara ifikapo Oktoba 05 mwaka huu huduma za awali ziwe zimeanza kutolewa na kuahidi kwamba wizara yake itafanyia kazi suala la upungufu wa watumishi hasa kwenye sekta ya Afya.
Agizo jingine lilikuwa ni kwa Afisa Ardhi ambaye nae aliagizwa kuanza mchakato wa kubainisha uzio kwenye eneo hili la kituo cha Afya Nyakyanja.
Mh. Jafo alipata pia kutembelea zahanati ya Ihembe II iliyojengwa na wananchi wa eneo hilo kwa Ufadhili wa shirika la World Vision huku uongozi wa wilaya ukianishwa kwamba hospitali hiyo haijaanza kutumika kutokana na zuio la uongozi wa Idara ya Afya mkoa jambo ambalo kumsingi lilionekana kumshangaza sana naibu waziri na kuahidi kulifanyia kazi.
Ziara yake pia ilifika katika eneo la kijiji cha Ihembe I mahali ambapo shughuli ya uzinduzi wa ujenzi wa darasa moja na ofisi mbili za walimu kwa shule ya msingi Ihembe I ulifanyika.
Majengo hayo ni ujenzi uliofanywa na ndugu Philibert Rwakiromba ambaye ni Mhasibu katika ofisi ya Waziri wa nchi TAMISEMI Dodoma ujenzi uliotajwa kuanza mwaka 2015.
Katika risala yao uongozi wa kijiji ulibainisha suala la upungufu wa walimu, uhitaji wa kompyuta na printa na ubovu wa baadhi ya majengo ya madarasa katika shule hii ya kihistoria ambayo ilijengwa mwaka 1945.
Katika hotuba yake kwenye eneo hilo, Waziri Jafo alimwagiza mwakilisha wa Mkurugenzi wa Elimu TAMISEMI aliyekuwepo kwenye neo hilo kufanya ukarabati wa majengo ya madarasa kwa kuweka mabati mapya na kuwekeka madirisha na sakafu mpya.
Naye Kaimu Mhandisi wa ujenzi wa wilaya Karagwe Mhandisi Ludovick Mtagurwa aliagizwa kuanza kufanya tathmimi mapema kuanzia tarehe hiyo ya ziara.
Ziara ya Mh. Naibu Waziri ilimalizikia kwenye kituo rafiki cha vijana cha Angaza kwa Naibu Waziri kuzungumza na watumishi ambapo alisisitiza umuhimu wa kuchapa kazi kwa watumishi hao huku akiwaagiza wakuu wa Idara na Vitengo kuwasimiamia kikamilifu watumishi wote waliopo chini yao.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.