NAIBU WAZIRI WA UJENZI AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mh. Eliasi Kwandikwa amefanya ziara ya kikazi wilayani Karagwe kwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara ya Kyaka - Bugene pamoja na barabara zinazotekelezwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini (TARURA)
Akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Karagwe alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Timu ya wataalam wa Halmashauri na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, Mh. Kwandikwa aliwashukuru viongozi wilayani humu kwa mshikamano wanaounesha ambapo alisema mshikamano huo unaonesha kuwa viongozi wilayani hapa wanafanya kazi kwa umoja.
Hali kadhalika, Naibu Waziri Kwandikwa aliwaeleza wajumbe waliokuwa wakimsikiliza kwamba kukamilika kwa mtandao wa barabara na kutasaidia mazao ya kilimo kusafirishwa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Karagwe alipongeza hatua ya Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS Mkoa wa Kagera kwa kukarabati eneo la milima ya Kishoju na kuweka alama za tahadhali jambo alilolitaja kuwa limesaidia kupunguza ajali za mara kwa mara kwani hapo awali ilikuwa ni desturi kwa eneo kutokea kwa ajili kwa kila juma.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mh. Dawson Paulo alimwomba Naibu Waziri kuisadia Halmashauri ya Wilaya ili mkandarasi alijenga barabara kampuni ya CHICO kulipwa kwa ushuru wa huduma ambapo mkandarasi anadaiwa na Halmashauri.
“Nimelipokea hilo la ushuru wa huduma nitalifanyia kazi”, alisisitiza Mh. Kwandikwa
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.