Mradi wa CHSSP watambulishwa Wilayani Karagwe
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE
Community Health and Social Welfare Strengthening Program (CHSSP) ikiwa ni Program ya Uimarishaji Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na taasisi iitwayo John Snow inc (JSI) ambayo makao yake katika kanda ya Ziwa yapo jijini Mwanza mnamo siku ya Jumamosi ya tarehe 22 Julai, 2017 ilifanya mkutano wa utambulisho katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe lengo likiwa ni kuutambulisha mradi huu wa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania kupitia Wizara, Taasisi na Halmashauri na wadau mbalimbali ambapo muda wake wa utekelezaji ni kuanzia Novemba 2014 – Oktoba 2019.
Mradi huu wa CHSSP unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia shirika la USAID huku utekelezaji wake ikifanywa kupitia mashirika mawili yaani JSI (Taasisi ya Utafiti na mafunzo) na World Education Inc. unatarajia kuzifikia takribani Halmashauri 84 kwa muda huo wa miaka mitano ya utekelezaji.
Lengo kuu la Mradi huu ni kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za Afya ya jamii na ustawi wa jamii kwa makundi maalum na ya kipaumbele huku malengo mahususi yakiwa ni kuwezesha upatikanaji wa watoa huduma waliobora wa afya ya jamii na ustawi wa jamii pamoja na kuimarisha/kuwezesha utaratibu wa miundo, mifumo na ushirikishwaji wa asasi za kiraia katika kutoa huduma za afya ya jamii na ustawi wa jamii.
Katika lengo la kuwezesha upatikanaji wa watoa huduma waliobora wa afya ya jamii na ustawi wa jamii mikakati ya mradi huu ni kuhakikisha kuwa miongozo mbalimbali inahuishwa na kusambazwa kwa wadau ili kuweza kuchangia kuwafikia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, vijana wa kike walio katika balehe na WAVIU.
Mkakati mwingine ni uimarishaji na kupanua nguvu kazi ya ustawi wa jamii mpaka katika ngazi ya kijamii.
Katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya, kamati zitakazoundwa zitasaidia kusimamia na kuwezesha kuundwa kwa kamati za kata, kufanya usimamizi saidizi katika ngazi za chini na kutoa ripoti ya utekelezaji wa shughuli zilizopangwa huku kamati za kata zikitakiwa kufundisha na kutoa ushauri kwa kamati za vijiji na kutos ripoti ya utekelezaji wa shughuli kwenye kamati ya Halmashauri.
Kwa upande wa Kamati za vijiji, Timu itaratibu shughuli zote za VVU na UKIMWI katika kijiji na mtaa ikiwa pia na kutoa ripoti ya utekelezaji kwenye kamati ya kata.
Kwenye maeneo ambayo Program hii imeshatekelezwa mpaka sasa mafanikio kadhaa yameshafikiwa mpaka sasa ikiwemo kuleta mahusiano mazuri ya kikazi na serikali, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Tume ya Kudhibiti UKIMWI na Ofisi ya Raisi, TAMISEMI
Pia imeweza kufundisha wafanyakazi wa afya 219, kuwezesha mapitio ya mwongozo wa Kamati za UKIMWI na kuinua/kufufua mifumo ya kijamii katika serikali za mitaa.
Katika hatua ya kuelekea kuanza kutekelezwa kwa mpango huu, Bi. Edina Kabyazi, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Karagwe aliteuliwa kuwa mratibu wa “Focal person” huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe ndugu Godwin Moses Kitonka na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe Mh. Wallace Murokozi Mashanda wakisaini Mktaba wa Makuliano ya kufanya kazi (MoU) na Mradi huu wa CHSS.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.