Mkuu wa Wilaya, Baraza la Madiwani Waweka Mikakati Mizito Zao la Kahawa.
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE.
Mkuu wa Wilaya Karagwe Mh. Godfrey Mheluka na Baraza la Madiwani Wilayani hapa wameyapokea maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa aliyoyatowa mjini Dodoma mnamo tarehe 14Januari, 2018 kuhusu uendelezaji wa zao la kahawa kwenye mikoa inayolima zao hili ikiwemo Mkoa wa Kagera.
Akitoa maelezo hayo ya serikali kupitia kikao cha Baraza la Madiwani mnamo tarehe 30/01/2018, Mh. Mheluka aliwajulisha wajumbe wa kikao hicho ya kwamba serikali imedharia kwa dhati kabisa kuboresha kilimo cha mazao matano ya biashara ambayo ni kahawa, pamba, korosho, chai na tumbaku.
“Ndugu zangu tunapozungumza hapa tayari wananchi wa mikoa ya kusini wameanza kunufaika na zao la korosho ambapo kwa sasa korosho yao inauzwa kwa kilo moja takribani sh 4,000 likiwa ni ongezeko la zaidi ya sh.2,000”, alisisitiza Mh.Mheluka.
Aidha katika kikao hicho, Mh. Mheluka alitaja baadhi ya mikakati iliyofikiwa na serikali kupitia kikao hicho cha Waziri Mkuu na kile kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mh. Meja Jenerali(Mst) Salim Mustapha Kijuu kilichofanyika tarehe 28/01/2018 mjini Bukoba.
Kwa mujibu wa Mh. Mheluka baadhi ya maelekezo yaliyogusiwa kupitia kikao hicho yalihusisha kutambuliwa kwa wakulima wa kahawa ambapo maafisa ugani na watendaji wa kata waliagizwa kutekeleza kazi hii kikamilifu.
Maagizo mengine kwa ngazi ya mkoa na wilaya ilikuwa ni agizo la Afisa Kilimo mkoa kusimamia zao la kahawa kwa kushitikiana na Maafisa Kilimo na maafisa ugani kwenye ngazi ya Wilaya.
Aidha maafisa ugani walitakiwa kwenda vijijini na jingine lilikuwa ni kwamba kila kijji kiwe na chama cha msingi kitakachoratibiwa na chama cha ushirika ifikapo Februari 2018 na pia kila mkoa uliagizwa kuwa na ushirika wake.
Pamoja na agizo la Waziri Mkuu kuhusu Katibu Tawala wa Mkoa kusimamia wataalam wake, ajenda ya mazo matano ya biashara imeagizwa kuwa ajenda ya kudumu kwenye vikao vyote vya maamuzi katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya na mkoa kwa ujumla.
Jingine lilikuwa ni marufuku ya wafanyabiashara kununua moja kwa moja kwa wakulima kahawa badala yake iliagizwa kwamba kahawa zote zinunuliwe sokoni.
Agizo jingine ni kwamba gari lolote litakalokamatwa kujihusisha na kahawa litaifishwe.
Aidha maagizo mengine yalihusu Halmashauri ya Wilaya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya kahawa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya zitumike kudhibiti magendo kwenye maeneo yao.
Bodi ya kahawa isisimae majukumu ya mfuko wa kahawa na wakati huo huo wakuu wa mikoa wasiruhusu vikundi vingine isipokuwa ushirika na mikoa na wilaya ikutane na wadau.
Agizo jingine lilikuwa ni kwamba Halmashauri ya Wilaya hii kutunga sheria ndogo kuwadhibiti wakulima wazembe.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.