Mkuu wa Mkoa wa Kagera atema cheche Wilayani Karagwe
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu), Salum Mustapha Kijuu mnamo tarehe 27 Julai,2017 kupitia kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kwa ajili kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Serikali za Mitaa zilizoishia tarehe 30 Juni,2017 alitoa maagizo kadhaa kwa viongozi wa Halmashauri ya wilaya Karagwe yanayolenga kuimarisha mfumo wa uwajikaji na ukusanyaji wa mapato serikalini.
Maagizo yake haya yalilenga katika kuisaidia Halmashauri ya Wilaya Karagwe kutokukumbwa na Hati chafu ya ukaguzi wa Fedha unaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali katika kila kipindi cha mwisho wa mwaka na ikizingatiwa kwamba Halmashauri ya Wilaya Karagwe ilipata hati safi kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2015/2016.
Agizo lake la kwanza alilolitoa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe ndugu Godwin M. Kitonka, Mkuu wa Mkoa alioneshwa kutokuridhishwa kwake kwa namna Halmashauri za Mkoa wa Kagera zinavyojibu Hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu zaSerikali ambapo aliagiza kuimarishwa kwa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani ili kiweze kufanya kazi iliyokusudiwa.
Pia ilikuwa ni agizo la kuimarisha kamati za ukaguzi kwa kuziwezesha kufanya kazi kikamilifu ili kubaini thamani ya Fedha”Value for money” kwa kila mradi unaotekelezwa.
Suala jingine lilikuwa ni suala la ukusanyajiwa mapato ambapo Mkuuwa Mkoa aliagiza Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya ukusanyaji wa mapato kuliko kuendelea kukusanya kwa kutumia vyanzo vile vile kila wakati huku akisisitiza zoezi hili kwenda sambamba na suala nzima la ufungaji wa mfumowa ki-elektronikina vyanzo vyote vya mapato viingizwe kwenye mfumo huu ili kuboresha shughuli za ukusanyaji wa mapato.
Agizo jingine lilikuwa ni kwamba Halmasahuri zihakikishe zinafuaitilia mwenendo wa miradi ya maendeleo hasa ile ya Maji, barabara na UKIMWI iliiweze kukamilika kwa wakati. Na katika eneo hili Mkuu wa Mkoa aliamuru iwepo mipango kazi katika kufuatilia jambo hili.
Suala jingine lililogusiwa katika Hotuba hiyo ya Mkuu wa Mkoa ilikuwa ni juu ya Usimamizi wa mikataba ambapo aliiagiza menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya kuhakiksha kwamba inafanya uchambuzi wa mikataba ikiwemo kufanya marekebisho pale ambapo itaonekana kwamba miradi hiyo haina tija.
Alisisitiza juu ya azma ya Halmashauri ya Wilaya Karagwe kusimamia Mfuko wa Wanawake na Vijana huku akibainisha kwamba hali ya utekelezajiwa jambo hili si ya kuridhisha na kutoa wito kwa waheshimiwa madiwani kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa jambo hilo huku akishauri Halmashauri ya Wilaya kuungalia upya utaratibu wa kupeleka Fedha kwa vijana uwe ni awamu kuliko inavyofanyika sasa kwani kiasi cha fedha kinahopokelewa na vijana hao hakiwezi kuwawezesha katika kubuni kitu gani wafanye kutokana na ukweli kwamba wanahitaji mtaji mkubwa na Fedha wanayopata ni kidogo.
Alihitimisha hotuba yake kwa kuliomba Baraza la Madiwani ambacho ndiyo chombo cha juu cha maamuzi kwenye Halmashauri kuwa na meno zaidi katika kusimamia shughuli zote za maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya huku akiahidi kwenda kufuatillia kwa Meneja wa TRA Mkoa kuona kama kuna uwezekano wa kusogeza Huduma ya kusajili huduma ya Boda boda hapa wilayani ili kuwapunguzia gharama wananchi wanaosafiri umbali mrefu kwa kutoka Karagwe kwenda Bukoba kwa ajili ya shughuli hiyo ikiwa ni kujibu ombi lililotolewa na mbunge wa Karagwe Mh. Innocent Lugha Bashungwa kwa Mkuu wa Mkoa kupitia kikao hicho cha Baraza la Madiwani.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.