Mkuu wa Mkoa wa Kagera Afanya Ziara ya Kihistoria Wilayani Karagwe.
Na Innocent E.Mwalo, KARAGWE.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Meja Jenerali(Mst) Salim Kijuu amefanya ziara ya kihistoria Wilayani hapa kwa kukagua miradi ya maendeleo inayohusisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kayanga, Kituo cha Afya cha Nyakayanja na Zahanati ya Kafunjo pamoja na kuhimiza shughuli za maendeleo kwenye maeneo hayo ikiwemo suala la kilimo cha kahawa, uanzishwaji wa bustani za matunda pamoja na suala la lishe ili kuepukana na suala la utapiamlo linalotajwa kuzikumba familia nyingi katika mkoa wa Kagera.
Ziara yake hiyo ilianzia katika kituo cha Afya cha Nyakayanja ambapo ujenzi wake umekamilika kwa kiasi kikubwa ambapo katika kituo hicho Mkuu wa Mkoa aliweza kupata taarifa ya ujenzi wa mradi huo ulianza mnamo mwaka 2016 ambapo mpaka sasa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje iliyogharimu kiasi cha Tsh. 244,425,000.00, ujenzi wa nyumba ya watumishi uliojengwa kwa hisani ya World Vision kwa kiasi cha Tsh.70,900,000.00, ujenzi wa vyoo vya wagonjwa na kichomea taka ambapo kwa pamoja umegharimu kiasi cha Tsh. 12,055,000.00
Mkuu wa mkoa alioneshwa kugushwa na jitihada hizo za wananchi hasa katika kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo hayo na kuahidi kwamba serikali itatoa kiasi cha Tsh. 400,000,000.00 ili kuunga mkono jitihada hizo.
Baada ya ukkaguzi kwenye kituo hicho, msafara ulielekea katika kituo cha Afya cha Kayanga ambacho ndio kituo kikubwa cha Afya Wilayani hapa chenye uwezo wa kuhudumia wananchi takribani 2,400 mpaka 3,500 kwa mwezi ambapo ujenzi wa miundo mbinu yake unaendelea kwa kasi kubwa.
Awali katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa, Kamu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Adeodata Peter alielezea kuwa huduma katika kituo hiki imeimarika zaidi ya mara dufu ambapo idadi ya wanawake wanaojifungulia katika kituo hiki imeongezeka kutoka wanawake 40 na 45 ambao walikuwa wanajifungulia kwenye kituo hicho hapo awali hadi kufikia wanawake 110 na 140 kwa mwezi huku vifo vya akina mama vikipungua kutoka kutoka vifo 15 hadi vifo 05 ambayo ni sawa na asilimia 69.
“Ujenzi wa miundo mbinu unaoendelea katika kituo hiki cha afya hiki unalenga kutibu changamoto zilizoonekana hapo hapo katika eneo hilo lakini pia athali za tetemeko la ardhi lililotokea katika mkoa wa Kagera mnamo 10/09/2016 na kusababisha changamoto kadhaa ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya kituo hiki cha afya na makazi ya watu”, alibainisha ndugu Adeodata kupitia taarifa hiyo.
Ndugu Adeodata aliendelea kusisitiza kwamba kufuatia athari hizo za tetemiko la ardhi, Kituo hiki cha afya kilipokea kiasi cha Tsh.170,714,452.18 mnamo 16/06/2017 kutoka Mfuko wa Maafa wa Mkoa kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti na power house ambapo kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya Karagwe, Dkt. Libamba Sobo fedha hizo ziliweza kupelekwa moja kwa moja katika kituo hiki cha afya kwa ajili ya kutekeleza mradi huo kwa kutumia utaratibu wa “Force Account”
Aidha taarifa hiyo iliendelea kusisitiza kwamba kutokana na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama (Mb) aliyoitoa mnamo 11 -13 /07/2017 wilayani hapa na mkoani Kagera kwa ujumla, kituo cha Afya cha Kayanga kimeweza kupokea takribani kiasi cha 72,989,530 ikiwa ni kutekeleza ahadi yake hiyo juu ya urejeshwaji wa miundombinu hiyo kwenye kituo cha Afya cha Kayanga.
“Sio hivyo, Halmashauri ya Wilaya Karagwe imeweza kupokea pia kiasi cha Tsh. 500,000,000 kutoka Serikali kuu chini ya mradi wa kuboresha vituo vya afya ikiwa ni kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa majengo wa Kituo cha Afya cha Kayanga kwa ufadhili wa Serikali ya Canada”, alisisitiza ndugu Adeodata.
Aidha taatifa hiyo iliendelea kusisitiza kwamba tayari kuna vifaa vya ujenzi vilivyopokelewa kutoka ghala la maafa mkoa ni pamoja na mabati ya kuezekea 280, matofali ya block 8,600, wire Pv 2.5 mita 400 na wire pv 1.5 mita 500.
Kutokana na michango hiyo tayari tayari ujenzi wa mradi wa wodi ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti na power house ambapo ujenzi wake umekamilika kwa zaidi ya asilimia 92.3
Aidha ujenzi wa majengo mengine ambayo ni wodi ya akina mama, nyumba ya mtumishi, jengo la huduma za wagonjwa za afya ya uzazi na mtoto pamoja nahuduma za wagonjwa wa nje (OPD na RCH) na jengo la wodi ya wanawake umekamilika kwa asilimia 89.02.
“Itakumbukwa kwamba hapo awali kituo kilipokea Tshs. 743,704,057.20 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, ambapo fedha zilizokwisha kutumika ni Tsh.591,688,477.00 na zilizobaki ni Tsh. 152,015,580.20 ambazo zinaendelea kutumika ili kukamilisha ujenzi na ukarabati wa majengo yanayokusudiwa ambayo ni wodi ya wagonjwa, jengo la upasuaji, jengo la utawala, store ya dawa na jengo la CTC ambapo ujenzi wake unatajiwa kuanza mwezi huu”, ilisisitiza taarifa hiyo
Kituo hiki cha Afya Kayanga ni kituo pekee cha Afya kilichopo ndani ya Wilaya Karagwe ambacho kilianza kutoa huduma mwaka 1961 ambapo kilipoanza muda huo ilikuwa kama sehemu tu ya kutolea huduma ya kwanza (Health post) ambapo baadae kulipandishwa hadhi na kuwa kituo cha Afya.
Mambo yalipamba moto zaidi katika zahanati ya Kafunjo ambapo umati wa wananchi ulifurika katika kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambapo Mkuu wa Mkoa aliwapongeza sana wananchi wa maeneo hayo kwa kuchangia kiasi cha Tsh.5,735,000.00 katika ujenzi wa zzahanati hiyo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa alitumia fursa hiyo kwenye maeneo yote aliyoyatembea kuwahimiza wanachi kushiriki katika kilimo cha kahawa na ulimaji wa bustani za matunda na zaidi zaidi alihamasisha juu ya ulaji wa chakula bora ili kuepukana na tatizo la utapiamlo linalotajwa kuundama mkoa wa Kagera.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.