MIKAKATI YAWEKWA KUKUZA KILIMO CHA ZAO LA MIHOGO
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE
Madiwani wa Halmasahuri ya Wilaya Karagwe wamekubaliana kwa kauli moja kwenda kuhamasisha wananchi kwenye maeneo yao ili wananchi hao waweze kuupokea mradi wa zao za mihogo unaotajiwa kudumu kwa muda takribani miaka mitano katika mkoa wa Kagera huku wakulima 28 wakitarajiwa kunufaika na mradi huo mkoani hapa.
Mambo haya yalifikiwa kupitia maazimio yaliyowekwa na uongozi wa madiwani katika warsha iliyowashirikisha viongozi hao na timu ya wataalam kutoka katika Mradi huu unaotekelezwa na taasisi iitwayo Mennonite Economic Development Associates (MEDA) kwa kushirikiana na taasisi nyingine iitwayo International Institute of Tropical Agriculture (IITA) ambao makao yake makuu yapo jijini Dar es Salaam unalenga kuhakikisha unaboresha kilimo cha zao la mhogo kutokana na kuimarika kwa soko la zao hilo kwenye mataifa mengine duniani ikiwemo taifa la China.
Aidha wataalam hao waliweza kuainisha hitaji la kuletwa kwa mbegu za kisasa kwa zao hilo kwamba kutosaidia kukuza uzalisashaji wa zao hilo kutokana na mbegu zake kuhimili magonjwa.
Timu ya Wataalam ambao ndio pia walikuwa wawezesha katika warsha hii iliwahusisha Lokola Ndibalema na Devis Mwakanyamale wote wakitoka IITA.
Wengine walikuwa Heavenlight Somboi na Paul Enecko wote kutoka MEDA huku timu ya wataalam kutoka Wizara ya Kilimo ikiwahusisha Beker Chirimi, Consesa Bagambisa na Dkt. Deusdedith Mlay.
“Tunasisitiza Halmashauri itenge Bajeti kwa ajili kuweka mkazo katika zao hili la mhogo kwani kwa utafiti tuliofanya zao hili lina faida sana kwa wakulima ikiwemo kuongezeka kwa faida mara mbili au tatu kwani wakulima wanatumia mbegu mara moja tu huku wakivuna kwa takribani mara mbili mfululizo bila kutumia mbegu tena”, alisisitiza Dkt. Deusdedith Mlay
Aidha katika warsha hiyo uongozi wilayani hapa uliweka maazimio kadhaa ikiwemo kulifanya zao la mhogo kuwa mojawapo ya mazao ya biashara wilayani hapa ikiwemo kutengeneza sheria ndogo ya zao hili.
Maazimio mengine yalikuwa menejimenti ya Halmashauri ya wilaya kupokea wazo hili ili kila kata ilete orodha ya wakulima wa mhogo na lilitolewa ombi la kwa taasisi hizi za MEDA na IITA kutoa mafunzo kwa watendaji wa kata.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.