Mafunzo ya Mpango wa Bajeti yafanyika Wilayani Karagwe
Na Innocent E. Mwalo, Karagwe
Mafunzo ya Mpango wa Bajeti “PlanRep” katika Halmashauri ya Wilaya Karagwe yamefanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 21/09/2017 hadi tarehe 23/09/2017 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya huku wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri kila mmoja akihudhuria na msaidizi wake mmoja kwa lengo la kujifunza mfumo huu mpya ambao utakuwa ni kielektroniki ukilinganisha na ule mfumo wa zamani.
Mafunzo haya yalikuwa na wawezeshaji wa aina tatu yaani wawezeshaji wa kitaifa ambapo ndugu Michael D. Gunewe, ambaye ni Afisa Utumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya Morogoro aliwezesha.
Huku ndugu Joachim Nyanda ambaye ni mchumi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera kwa alikuwa ni mwezeshaji wa ngazi ya Mkoa akishirikiana na ndugu Robert Mhongole ambaye ni mchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka taasisi ya kuimarisha mifumo ya Mawasiliano serikalini yaani PS3.
Wawezeshaji wa ngazi ya wilaya walikuwa ni Afisa TEHAMA wilaya, ndugu Beatus Nyarugenda, Afisa Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, ndugu Herbert Bilia na Katibu wa Afya, ndugu Josephat Nkebukwa ambao kwa pamoja walipata mafunzo haya jijini Mwanza mwishoni mwa mwezi Julai, 2017.
Awali akifungua mafunzo hayo, Bi. Ashura Kajuna, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji aliyekuwa katika majukumu mengine ya kikazi Mkoani (Bukoba) alisisitiza suala la nidhamu katika kufuatilia mafunzo hayo muhimu.
Katika siku hizo tatu za mafunzo hayo washiriki wapatao 39 walipata nafasi ya kujifunza mada mbalimbali zikiwemo zile za kuingiza taarifa mbalimbali kwenye mfumo huu mpya wa Mpango wa Bajeti.
Mafunzo haya yalihitimishwa tarehe 23/09/2017 huku Bi. Adeodata A. Peter (Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya), Ndg. Herbert Bilia, Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji na Mweka Hazina, Ndg W.V. Swai wote kwa pamoja wakimshukuru sana Mwezeshaji Kitaifa, Michael D. Gunewe kwa kazi nzuri alioifanya katika zoezi hilo huku wakiahidi kwamba mafunzo haya yatafanyiwa kazi zaidi kabla ya shughuli rasmi ya bajeti kama ilivyokusudiwa na serikali ambapo naye ndg. Gunewe alipopata nafasi ya kuaga aliwashukuru washiriki kwa usikivu na ushirikiano wao waliouonesha wakati wote wa mafunzo
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.