Na Frank I. Ruhinda
Madiwani wakishirikiana na timu ya wataalamu kila mtu kwa nafasi yake kwa kauli moja wameazimia kuhakikisha wanapokea kiasi cha wanafunzi elfu moja mia saba na ishirini wa kidato cha kwanza mwezi januari bila kukosa hata mmoja.
Wameagiza Wah Madiwani waitishe vikao vya WDC vya dharula kila diwani kwenye kata yake, ili kubaini idadi ya wanafunzi watakao ingia kidato cha kwanza, mapungufu ya vyumba vya madarasa na madawati yanayohitajika ili viendane.
Azimio hilo, lilitolewa kwenye kikao cha baraza la madiwani cha dharula, baada ya Mh mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Wallace Mashanda kuombwa kufungua kikao hicho, ambacho kilikuwa na agenda moja ya kutenga mipaka ya mji mdogo wa Kayanga Wilayani Karagwe.
“Wah Madiwani kabla ya kufungua kikao hiki naomba niseme kuwa, mwezi januari tunakusudia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, wapatao 1720, lakini kwa mazingira ninayoona sioni kama tutaweza kwani vyumba vya madarasa havitoshi na shule nyingine hazina madawati hadi kufikia wanafunzi kukaa chini” alisema.
Aidha azimio hilo, liliwataka Wah Madiwani wote waitishe vikao vya WDC kwenye kata zao, wakishirikiana na watendaji wa kata, wakuu wa shule na watendaji wengine, ili kuhakikisha wanakamilisha vyumba vya madarasa na kutengeneza madawati ya kutosha kulingana na idadi ya wanafunzi wanaohitajika katika shule husika.
“Hivi jamani hatuwezi kuona aibu, kwani ni juzi tulikuwa tunafanya shughuli za wiki ya elimu katika shule st peter clavery, iliyokuwa ya kwanza kitaifa katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka jana, lakini mwaka huu imekuwa ya kumi na mbili na hatujui mwaka ujao, pia Wilaya yetu ikiwa ya mwisho kimkoa” alisema.
Baada ya azimio hilo, mwenyekiti alifungua kikao na kujadili agenda yao ya kutenga mipaka ya mji mdogo wa Kayanga, na kukubaliana kuongezewa maeneo kwa baadhi ya kata mfano Kayanga na Bugene ile hali kata nyingine kupunguziwa maeneo kama vile Ndama na Nyakahanga.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.