Jambo Bukoba, Wadau wa Maendeleo Wafanya Tathmini ya Miradi ya Jambo Bukoba Wilayani Karagwe.
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE.
Timu ya Jambo Bukoba ikiongozwa na Meneja mradi huo ndugu Gonzaga Stephen mnamo Desemba 07, 2017 walifika wilayani hapa ambapo kwa kushirikiana na wadau wa maendeo yaani mradi wa Jambo Buboba waliweza kufanya kazi ya tathmini ya kina juu ya namna miradi hiyo ilivyotekelezwa tangu ilipoanzishwa Shirika la Jambo Bukoba lilipoanza kufanya kazi mnamo mwaka 2008.
Kwa upande wa Halmasahuri ya Wilaya Karagwe ujumbe wa Timu ya Tathmini uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya Karagwe, Mh. Dawson Paulo Byamanyirwohi akishirikiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, ndugu Ashura Kajuna.
Wengine walioshiriki katika tukio hilo walikuwa ni waheshimiwa madiwani ambao mradi huu ulitekelezwa kwenye maeneo yao, wataalam kutoka Idara ya Elimu Msingi akiwemo Afisa Utamaduni wa Wilaya ndugu Alloyce Mujungu.
Pia walikuwepo waratibu Elimu kata, walimu wakuu, walimu wa michezo na baadhi ya wajumbe wa kamati za shule kutoka katika maeneo hayo ya utekelezajiwa mradi.
Jambo Bukoba ni mradi ulianzishwa na ndugu Clemens Mulokozi mwaka 2008 kwa lengo la kuendeleza vipaji vya watoto katika shule za msingi Tanzania kupitia michezo ukiwa na lengo la kuhasisha usawa wa kijinsia, kuboresha Elimu na afya lengo likiwa kundi la watoto wa shule wa mpaka miaka 14.
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Meneja Mradi wa Jambo Bukoba, ndugu Gonzaga Stephen kwa kipindi cha takribani miaka tisa ambayo Jambo Bukoba wamefanya kazi wilayani Karagwe tayari wameshafadhili miradi yenye thamani ya kiasi cha sh. 23, 755,562 huku mchango wa wananchi ukiwa ni kiasi cha sh.10,928,377.
“Na katika utekelezaji wa maradi huo tumeweza jumla ya wanafunzi 2710 wameweza kunufaika na mradi huo huku Elimu ya michezo ikizifikia shule takribani 98 kati ya shule 118 zilizopo Wilayani hapa ikiwa ni sawa na 85.25%”, alisema ndugu Gonzaga.
Aidha ndugu Gonzaga aliitaja miradi hiyo iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa darasa katika shule ya Msingi Karalo, ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya Msingi Bugene, ujenzi wa ofisi ya walimu katika shule ya msingi Ihanda.
Miradi mingine ni ujenzi wa tank la maji katika shule ya msingi Maguge na ujenzi wa mashimo ya choo katika shule ya Msingi Ahakishaka.
Aidha katika maeneo mengi kwenye shule hizo 98 waliweza kugawa mipina na vifaa vingine vya michezo.
Kwa upande wao baadhi ya walimu waliopata kuchangia katika tahtmini hiyo walizitaja faida zilizopatikana katika Elimu kutokana na ufadhili wa Jambo Bukoba kuwa ni kuinua kiwango cha ufaulu, walimu kupewa mafunzo, kujengwa kwa miradi ya maendeleo katika sekta za Elimu na Afya, shule kupewa vifaa vya michezo na kufanyika kwa kampeni mbalimbali kuhusu masuala ya UKIMWI.
Faida nyingine iliyotajwa ilikuwa ni kuongezeka kwa ufaulu hasa kwa somo la Hisabati kutokana na michezo ya maumbo inayochezwa na wanafunzi mashuleni.
“Pamoja na mafanikio haya lakini bajeti michezo bado ni changamoto na nitoe wito kwenu ninyi wadau kuifanyia kazi changamoto hiyo”, alisikika Audax Ndaula, Mratibu Elimu wa kata ya Ndama.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mh. Dawson Paulo Byamanyirwhohi aliwashukuru Jambo Bukoba kwa ufadhili wao wa miradi hiyo na akatoa wito kwa wataalam wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwepo kwenye kikao hicho cha Tathmini kuwa mabalozi katika suala la bajeti ili mchakato huo utakapoanza basi Halmashauri ya Wilaya iweke katika mipango yake bajeti ya semina ya michezo kwani mradi wa Jambo Bukoba ufadhiliwa wake umefikia kikomo.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.