Idara ya Zima Moto Wilayani Karagwe yawezeshwa
Na, Geofrey A.Kazaula – Karagwe
Kikosi cha zimamoto Wilayani Karagwe kimeongezewa nguvu baada ya kupata msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya takribani Millioni 30 za kitanzania.
Kwa mujibu wa Mkuu wa jeshi la zimamoto Wilayani Karagwe Sgt Peter Mmbare vifaa hivyo vimetolewa na wafadhili kutoka nchini Ujerumani kwa kushirikiana na Idara ya zimamoto ya jimbo la Kolon nchini humo.
Akitoa ufafanuzi juu ya msaada uliotolewa Sgt Peter ameeleza kuwa vifaa hivyo ni pamoja na Safety Belt, Fire Suit, Fedha tasilimu ambazo ni Euro 200 pamoja na Safety but kama mavazi maalum kipindi cha kuzima moto.
Aidha ameongeza kuwa wafadhili hao wame ahidi kuendelea kukisaidia kikosi cha zimamoto Wilayani Karagwe na kwamba kwa sasa wako kwenye mpango wa kununua gari kubwa kwaajili ya shughuliza zimamoto ambalo pia litakabidhiwa .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karagwe ndg, Godfrey Mheluka alipongeza jitihada zilizofanywa na wafadhili hao kwa kukisaidia kikosi cha zimamoto na kusisitiza kuwa vifaa hivyo vitumike katika kukabiliana na majanga ya moto.
Makabidhiano hayo ya vifaa yaliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karagwe yalihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali zikiwemo taasisi binafsi , wah Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi Ashura Kajuna, Katibu tawala na viongozi wengine ambao pia ni wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.