Na, Geofrey A. Kazaula
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imeibuka na Hati safi baada ya Ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG) Kwa kipindi cha mwaka 2015/2016.
Kwa mujibu wa Idara ya Fedha na Biashara ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Miongoni mwa sababu zilizopelekea upatikanaji huo wa hati safi ni pamoja na Halmashauri kusimamia vizuri sheria ya manunuzi pamoja na ufungaji mzuri wa vitabu uliozingatia kanuni na taratibu za fedha za Serikali za Mitaa.
Akifafanua vizuri juu ya Upatikanaji wa hati Safi kwa Halmashauri, Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara Ndg, Edward Malima ame eleza kuwa hati hiyo imekuja ikiwa ni matokeo ya ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi, viongozi wa ngazi mbalimbali katika Kata na Vijiji , Baraza la Madiwani pamoja na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ( CMT) ambapo kwa kupitia vikao vya kisheria, taratibu za manunuzi zili simamiwa vizuri Pamoja na Matumizi Mazuri ya Fedha za Serikali kwa mujibu wa Sheria.
Wilaya ya Karagwe ni miongoni mwa Wilaya 8 Za Mkoa wa Kagera na kwa sasa Halmashauri inaendelea kutekeleza usimamizi mzuri wa Matumizi ya Fedha kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha hati safi zinaendelea upatikana.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.