Na Frank I.Ruhinda
Imeshauriwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Karagwe iandae utaratibu wa kuwatoza ushuru wauza mkaa badala ya kuwaachia watendaji wa kata na vijiji ambao hawana jinsi wala sheria ndogo ya kuwalinda wakati wakiwa katika zoezi hilo.
Uhauri huo umetolewa na Mh diwani wa kata ya Nyakahanga Chalse Bechumila akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi katika kata za Kayanga, Nyakahanga, Ndama, Kituntu, Rugera na Kihanga ambapo ziara hiyo imekutana na wauza mkaa wakizurura mitaani kwa wingi.
Mh Bechumila amesema sheria inawataka wauza mkaa kulipia ushuru kiasi cha shilingi elfu kumi na mbili, lakini kwa mazingira ya kwetu ata ukiwatoza kiasi cha shilingi elfu tatu tu zinatosha kulingana na bei iliyoko sokoni na hali ya upatikanaji wa bidhaa hiyo.
“Inasikitisha kuona watu wetu wanakata miti kwenye mapoli yetu ya asili na baada ya kukata miti hiyo wala hawajikumbushi kupanda miti mingine huku wakishafikisha biashara yao sokoni bei wanajipangia wao wenyewe na halmashauri ambayo ndio mmiriki wa ardhi na misitu haipati chochote kutokana na ushuru wa biashara hiyo” alisema.
Nivyema kama halmashauri ingeandaa utaratibu wa kuwa na sheria ndogo ambayo itawapa watendaji wa kata na vijiji nguvu za kusimamia zoezi hilo aidha kwakutumia mgambo au laah wauzaji wenyewe kuja kulipia ofisini bila kuanza kukimbizana mtaani.
Mh. Bechumila amesema wakiamua kuwatoza elfu kumi na mbili kama inavyawataka sheria mama, wafanya biashara hao wataishia kuwakimbia wasimamizi wa sheria bila tija yoyote na ata wengine watashindwa kufanya biashara hiyo na kuwaachisha ajira yao.
Amesema hiki ni chanzo cha mapato kizuri kwa halmashauri na pia ni ajira kwa vijana wetu walioko mtaani ambao hawana ajira, japo inastahili wapewe kaufahamu kidogo kwa wale wakataji miti ili baada ya zoezi la ukataji basi wapande miti mingine siyokuacha vipara ambavyo matokeo yake ni jangwa.
Kwenye maeneo ya mji mdogo wa Kayanga, Omurushaka na Nyakahanga, gunia kubwa la mkaa linauzwa kufikia elfu kumi na saba na kumi na sita, kwenye maeneo mengine yenye vistesheni bei inapungua hadi kufikia elfu kumi na nne.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.