HALMASHAHURI YA WILAYA KARAGWE YAPATA HATI SAFI UKAGUZI ULIOFANYWA NA “CAG” KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE
Baraza la Madiwani kupitia kikao chake kilichoketi hivi karibuni katika ukumbi wa Vijana Rafiki Angaza kwa wamepokea na kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali, CAG za kuishia Juni 30, 2017 huku taarifa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, ndugu Godwin Kitonka katika Baraza hilo ya kwamba Halmashauri ya Wilaya hii imepata “Hati Safi” katika ukaguzi huo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mh. Godfrey Mheluka, alipongeza hatua hiyo huku akiainisha mambo kadhaa ambayo Halmashauri inatakiwa kuyafanyia kazi ili kuondokana na Hoja za Mkaguzi kwa siku za usoni.
Baadhi ya mambo yaliyosisitizwa na kiongozi huyo yalikuwa ni pamoja na Halmashauri kuhakikishia ya kwamba inaweka jitihada katika kukamikisha ujenzi wa nyumba ya watumishi katika chuo cha Ualimu cha Karagwe.
Jambo jingine lililo agizwa kwa uzito na kiongozi huyo ilikuwa ni Halmashauri ya Wilaya na hasa Menejimenti kusimamia kikamilifu suala la kukusanya mapato na pamoja na kukiwezesha kikamilifu Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kwa ajili ya kukiwezesha kutekeleza majukumu yake yatakayosaidia kurekebisha dosari kadhaa zinazoweza kuzuilika kabla ya ukaguzi unaofanywa na wakaguzi wan je kila mwisho wa mwaka wa Fedha.
“Kuhusu kujirudia rudia kila mwaka kwa hoja ya kutokurejeshwa kwa mikopo ya vikundi vya vijana na wanawake, napenda kuwaagiza Menejimenti kuyaleta majina hayo kwanza kwenye Ofisi yangu ili tuweze kusaidia pale inapowezekana ili kama ikishindikana basi wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya dola”, alisisitiza Mh. Mheluka.
Katika kikao hicho kilichoendeshwa kisayansi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mh. Wallace Mashanda wajumbe walijadili jumla ya Hoja 108 ikiwa ni pamoja na Maagizo ya Kamati ya Bunge (LAAC) manne, Hoja za nyuma yaani mwaka 2011- 2016 zikiwa ni 71 na Hoja zingine 51 zilizoibuliwa katika ikaguzi uliofanywa na CAG kwa mwaka 2016/2017
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.