Na, Geofrey A. Kazaula
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr Bashiru Ally amepokelewa kwa kishindo katika Wilaya ya Karagwe ambapo pia mapokezi hayo yalihusisha Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ambapo wote walijumuika katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ili kumpokea kiongozi huyo na kupokea maelekezo mbalimbali ya chama na Serikali.
Akiongea na Viongozi wa Chama na Serikali katika Ukumbi wa CCM Karagwe , kiongozi huyo aliwataka watendaji wa chama wote kufanya kazi kwa ufanisi ili kuyafikia matarajio ya CCM.
Alieleza kuwa uataratibu wa kukutana na watendaji wa Halmashauri tatu kwa pamoja ni mzuri licha ya kuwa ni gharama.
‘‘ Utaratibu huu wa kukutanisha Halmashauri tatu kwa wakati mmoja ni utaratibu mpya na ni mzuri licha ya kuwa unagharama lakini hakuna namna’’ alisema kiongozi huyo.
Aidha, aliwakumbusha viongozi juu ya Masharti ya mwana CCM ambayo ni pamoja na Kuheshimu watu huku akimtolea mfano Mwl Nyerere kuwa aliheshimu watu katika kipindi chake chote.
Ame eleza pia kuwa Masharti mengine ya mwana CCM ni pamoja na kuwa mtu anayefanya juhudi ya kuielewa na kuieleza itikadi ya CCM, kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha utu na kuwa mtu anayependa kushirikiana na wenzake .
Ame sisitiza juu ya kuamini katika ushirika na kuimarisha ushirika ili kuwainua wakulima kwani bila kufanya hivyo nguvu za wakulima huishia kunyonywa na walio wachache.
‘‘ Nitoe wito kwa wananchi wote kuhakikisha wanasimamia vizuri ushirika na wanajiunga katika ushirika ili kuhakikisha Kilimo kinakuwa na tija kwa wakulima kama yalivyo matarajio ya Serikali’’ alisema kiongozi huyo.
Kwaupande wake Naibu waziri wa Kilimo , Umwagiliaji na Ushirika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mh, Innocent L. Bashungwa aliwahakikishia wananchi kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera wanaendelea kufanya uchambuzi ili kubaini nyongeza halisi anayopaswa kupatiwa Mkulima wa Kahawa baada ya malipo ya awali yaliyokwisha fanyika.
‘‘ Naomba kuwatoa wasiwasi wakulima kuwa suala ya nyongeza katika malipo ya Kahawa yaliyokwisha fanyika awali linaendelea kushughulikiwa na Ofisi yangu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa na nyongeza hiyo italipwa baada ya kufanya uchambuzi na kujiridhisha juu ya kiasi halisi anachopaswa kupokea Mkulima,’’ alieleza kiongozi huyo.
Dr. Bashiru amewataka viongozi wa Chama na Serikali kuyatanguliza maslahi ya Taifa kwanza na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni sambamba na kuendelea kuitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.