“Chanjo ya Mbwa ni lazima”, asema Kitonka
Na. Innocent Mwalo, KARAGWE
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe, ndugu Godwin Kitonka amewaagiza wananchi wote wanaofuga mbwa wilayani humo kuhakikisha kwamba mbwa wao wanapata chanjo ya kuwakinga na ugonjwa wa kichaa cha mbwa, zoezi linalotarajiwa kuanza mapema jumatatu ya tarehe 10/07/2017.
Kitonka ameyasema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyosainiwa Julai 06, 2017 na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo redio za kijamii zilizopo wilayani humo.
Katika tangazo hilo, Kitonka amenukuliwa akisema zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku saba yaani litaanza tarehe 10/07/2017 na kumalizika tarehe 17/07/2017 huku zoezi hilo likitarajiwa kuendeshwa na maafisa mifugo katika kata zote za wilaya hiyo.
Tangazo hilo limeanisha pia gharama za kuchanja kila mbwa mmoja kuwa ni kiasi cha shilingi elfu mbili tu (2,000/=)
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amewaomba wananchi wa maeneo yote ya wilaya Karagwe kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo muhimu kwani madhara ya kutokuchanja mbwa ni makubwa katika ustawi wa jamii ya watu wa Karagwe.
Amesisitiza kuwa hatua kali kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaokiuka agizo hilo.
Itakumbukwa kwamba chanjo ya mifugo ikiwemo mbwa imekuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini lengo likiwa kuikinga mifugo kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayoikumba mifugo hiyo
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.